Ugomvi wa kisiasa baina ya jimbo la Iraq la Kurdistan na eneo lilobaki la Iraq, umezidi kuwa mkali.
Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Iraq,
Hoshyar Zebari, mwanasiasa maarufu kabisa wa Kikurd katika serikali ya
Iraq, ameiambia BBC kwamba Waziri Mkuu Nouri Al Maliki lazima aombe
msamaha na abadilishe kauli yake kuhusu Kurdistan.
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SIASA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SIASA. Onyesha machapisho yote
Julai 12, 2014
TAZAMA UKATILI HUU:MTOTO AFICHWA UVUNGUNI KWA MIAKA 6 MOROGORO
Posted on Jumamosi, Julai 12, 2014 by Unknown

Wakati
jamii ikiwa bado haijasahau mateso aliyoyapata mtoto Nasra Mvungi na
kusababisha kifo chake, tukio lingine la aina hiyo limetokea katika
Kijiji cha Matongola, Tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa, baada ya
kubainika mtoto wa miaka sita akiwa amefichwa uvunguni mwa kitanda na
kufanyiwa vitendo vya kikatili na mama yake mzazi.
Juni 22, 2014
BREAKING NEWS!!! DALADALA ZA GONGANA NA KUUWA WATU 19 DAR LEO HII.
Posted on Jumapili, Juni 22, 2014 by Unknown
Juni 16, 2014
Habari Picha: zilizochapishwa za mauaji Iraq.
Vuguvugu la Sunni lenye msimamo mkali la ISIS ambalo limeteka maeneo ya Kaskazini mwa Iraq limesambaza picha ambazo zinaonyesha jinsi wapiganaji wake walivyoangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa Iraq.
Habari Mbaya Kutoka Kenya,Watu 48 wauawa Usiku wa Kuamkia leo
Posted on Jumatatu, Juni 16, 2014 by Unknown
Watu wanaoshukiwa kuwa
wapiganaji wa Kiislamu wameshambulia kituo cha polisi na mahoteli na
vijiji mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .
Makabiliano makali yameripotiwa sehemu kubwa ya
Jumapili usiku huku wakaazi wakitorokea maeneo ya msitu karibu na kisiwa
cha Lamu..Juni 10, 2014
TAZAMA PICHA NA HABARI:WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGON, DC
Posted on Jumanne, Juni 10, 2014 by Unknown
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Mkuu wa Utawala na
Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka siku ya
Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake
walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo mtaa wa 22,
jijini Washington, DC.
Juni 09, 2014
Hiki ndicho Kilichosemwa bungeni juu ya picha chafu zinazosambazwa mitandaoni za watu maarufu.
Posted on Jumatatu, Juni 09, 2014 by Unknown
Mei 27, 2014
HABARI PICHA:POLISI WAUA TENA MAJAMBAZI TEMEKE
Posted on Jumanne, Mei 27, 2014 by Unknown
Mei 26, 2014
HII NI TAARIFA KUHUSU JESHI LA NIGERIA KUBAINI WALIKOFICHWA WASICHANA WALIOTEKWA
Posted on Jumatatu, Mei 26, 2014 by Unknown
Jeshi la nchini Nigeria limesema
linajua mahali walikofichwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa wakiwa
shuleni lakini hawawezi kuitaja sehemu hiyo hadharani.
Wasichana hao walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo
linadai haliwezi kuwaachia hadi watakapobadilishana wafungwa wao na
serikali ya nchi hiyo.
MBEYA CITY WACHAPWA 2-1 NA FC LEOPARD
Posted on Jumatatu, Mei 26, 2014 by Unknown
Mbeya City Usiku huu imefungwa Bao 2-1 na AFC Leopards ya Kenya katika Mechi yao ya Pili ya KUNDI B la Mashindano ya CECAFA NILE BASIN CUP iliyochezwa huko Khartoum, Sudan.
Hadi Mapumziko, Mbeya City walikuwa nyuma kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Mudde Musa katika Dakika ya 30 na Were Paul, Dakika ya 35.
Bao la Mbeya City lilifungwa na Deus Kaseke katika Dakika za Majeruhi.
Kwenye Mechi ya Kwanza, Mbeya City waliifunga Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 na Mechi yao ya mwisho ya KUNDI B ni hapo Jumatano dhidi ya Enticelles ya Rwanda.
KUTOKA IRINGA MJINI:CHADEMA WATIMULIWA KATIKA MAZISHI YA DEREVA BODA BODA , WASEMA WAO SI CHAMA CHA SIASA
Posted on Jumatatu, Mei 26, 2014 by Unknown
Mei 21, 2014
Soma hili:Tapeli Sugu akamatwa Nje ya Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma,Huyu hapa.
Posted on Jumatano, Mei 21, 2014 by Unknown

Mei 20, 2014
Picha Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa:fanyakazi Hodari wa Wizara na Wafanyakazi Bora wapokea vyeti vyao
Posted on Jumanne, Mei 20, 2014 by Unknown
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Batholomeo Jungu.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu,
Januari 20, 2014
HATIMAYE BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LATANGAZWA....UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI WAPYA..SOMA ZAIDI HAPA
Posted on Jumatatu, Januari 20, 2014 by Unknown
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue ametangaza baraza jipya la mawaziri wakiwemo walioziba nafasi tano zilizokuwa wazi na wengine kuhamishiwa wizara nyingine!
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue ametangaza baraza jipya la mawaziri wakiwemo walioziba nafasi tano zilizokuwa wazi na wengine kuhamishiwa wizara nyingine!
Januari 09, 2014
Desemba 18, 2013
TAZAMA TZ KAMA KENYA: ABIRIA YOYOTE ATAKAYE KUTWA AMESIMAMA KWENYE DALADALA KUTOZWA FAIN...!!!,"SOMA HAPA ZAIDI"
Posted on Jumatano, Desemba 18, 2013 by Unknown
POLISI Kikosi cha Usalama Barabarani, inaandaa sheria itakayosaidia kudhibiti ujazaji wa watu kwenye magari ya abiria, ambayo abiria atakayekutwa amesimama, atatozwa faini.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Desemba 09, 2013
MABOMU YALINDIMA MKUTANO WA DR SLAA KIGOMA,"SOMA HAPA ZAIDI"
Posted on Jumatatu, Desemba 09, 2013 by Unknown
JESHI la Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma, jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi ili kumnusuru Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa asifanyiwe fujo. Habari za uhakika kutoka Kasulu zinasema, Dk. Slaa alijikuta katika wakati mgumu baada ya kundi la vijana wanaokadiriwa kuwa kumi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuzua fujo.
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa asifanyiwe fujo. Habari za uhakika kutoka Kasulu zinasema, Dk. Slaa alijikuta katika wakati mgumu baada ya kundi la vijana wanaokadiriwa kuwa kumi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuzua fujo.
Desemba 06, 2013
TAZAMA MAZISHI YA NELSON MANDELA KUVUNJA REKODI,"SOMA ZAIDI HAPA"
Posted on Ijumaa, Desemba 06, 2013 by Unknown
Afrika na dunia inatarajiwa kushuhudia kitu kipya katika maziko ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95) aliyefariki dunia juzi, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi sita.
Serikali ya Afrika Kusini imesema kiongozi huyo ambaye atazikwa Desemba 15, imeandaa mazishi ya kihistoria yanayosemekana yatazidi yale ya Papa John 11.
Matukio ya shughuli mbalimbali zinazohusu mipango ya maziko ya kiongozi huyo maarufu yanatarajiwa kushuhudiwa sehemu mbalimbali duniani, tofauti na tukio jingine lililowahi kutokea barani Afrika mbali na kombe la dunia.
Rais Jacob Zuma alisema jana kwamba “Mpendwa wetu Madiba atazikwa kwa heshima zote za Serikali. Nimeagiza bendera zote za Afrika Kusini zipepee nusu mlingoti na hiyo itaendelea hivyo hadi tutakapokamilisha mazishi yake.
Mazishi ya Mandela yanalinganishwa na yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo yalihudhuriwa na wafalme watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais wapatao 70 na mawaziri kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili. Yanakadiriwa pia kulingana na maziko ya Winston Churchil aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza mwaka 1965.
Marais wote wa Marekani walio hai wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo iwapo afya zao zitawaruhusu kusafiri, pamoja na Prince Charles wa Uingereza na hata Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Pia watu maarufu wenye urafiki wa karibu na Mandela akiwamo msanii Oprah Winfrey wameshathibitisha kuhudhuria.
Changamoto la kiusalama
Kutokana na idadi kubwa ya wakuu wa nchi na watu maarufu duniani wanaotarajiwa kufika Afrika Kusini, suala la usalama limeelezewa kuwa changamoto mpya kwa vyombo vya usalama nchini humo.
Afrika Kusini imekuwa moja ya nchi zinazokabiliwa na matukio ya uporaji na mauaji yanayotokana na idadi kubwa ya wahalifu, wengi wao wakidaiwa kuwa wahamiaji haramu.
“Huyu ni shujaa wa dunia. Tutafanya mipango ya mazishi makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa. Nadhani kila nchi itakuwa imeandaa utaratibu wake wa namna ya kushiriki,” alisema mmoja wa wanadiplomasia wa Afrika Kusini ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Siku 11 za maombolezo
Serikali ya Afrika Kusini, kwa mujibu wa gazeti la The Guardian tayari imeweka wazi ratiba ya siku 11 za maombolezo tangu alipofariki dunia juzi jioni. Japokuwa ratiba hiyo ilishaandaliwa karibu mwaka mmoja uliopita na kupitiwa na kufanyiwa maboresho katika baadhi ya maeneo, inaonyesha namna maofisa wa Serikali ya Afrika Kusini walivyolipa uzito suala hilo na kulifanya kuwa tukio la kukumbukwa katika historia.
Mwannchi
Mwannchi
HII NDIYO KAULI YA MH. ZITTO KUHUSU WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUTANGAZA MSHAHARA WAKE BILA SHURUTI,
Posted on Ijumaa, Desemba 06, 2013 by Unknown
Picha ya zito kabwe
- WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA.
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, amesema mshahara wake kwa mwezi ni sh. milioni sita hivyo watu wanaosema analipwa zaidi ya hizo, wanalengo la kutaka kuharibu jina lake.
Pinda aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo akionesha kushangazwa na watu wanaodai analipwa sh. milioni 30 kwa mwezi.
"Hizi ni njama za watu wachache wanaotaka kuharibu jina langu, wanasema najiita Mtoto wa Mkulima wakati nalipwa sh. milioni 30 kwa mwezi si kweli...nalipwa sh. milioni sita tu ambayo ni pamoja na posho," alisema.
Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ole, Bw. Rajabu Mbarouk Mohammed (CUF), juu ya mchakato wa vitambulisho vya Taifa kukamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015, Bw. Pinda alisema hadi sasa mchakato huo unaendelea vizuri.
"Pamoja na kuchelewa kwake, Serikali imeweza kujitahidi ili kuhakikisha unakwenda vizuri kwa kuwafikia watu wote," alisema.
Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, amewataka wabunge kuacha kutanguliza masilahi ya vyama vyao ndani ya Bunge badala yake watangulize masilahi ya Taifa kwa manufaa ya Watanzania wote.
Bi. Makinda aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana wakati wa kipindi cha kuchangia Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni Mwaka 2013.
"Wabunge mnapaswa kuacha tofauti zenu za kichama ndani ya Bunge ambalo ni chombo muhimu cha kujadili maendeleo ya Taifa na wananchi wake...lipo tatizo la ushabiki wa vyama ndani ya Bunge hasa chama kimoja kinapowasilisha hoja, tunadili kwa pamoja kuijenga nchi yetu," alisema.
Akichangia muswada huo, Mbuge wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda (CHADEMA), alisema mchakato wa maandalizi ya kura za maoni si mzuri.
"Ni muhimu jamii ipewe elimu ya kutosha...kama muswada huu utapita, tuhakikishe vituo vya upigaji kura za maoni vinakuwepo ndani na nje ya nchi ili kutoa fursa kwa Watanzania waishio nje kupiga kura kama wenzao waliopo nchini," alisema.
Naye Mbunge wa Mbozi Magharibi, mkoani Mbeya, Bw. David Silinde (CHADEMA), alisema ni vyema Serikali ianze kuboresha daftari la kudumu kabla ya kuanza mchakato huo kwani kuna Watanzania wengi ambao majina yao hayapo katika daftari.
Alisema haziungi mkono Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Bara (NEC) na ile ya Zanzibar ZEC kupewa jukumu la kusimamia mchakato huo badala yake waachiwe wananchi wenye vigezo waombe kusimamia kura za maoni wakiwemo walimu.
Muswada huo uliwasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera ,Uratibu na Bunge), Bw. William Lukuvi. -- - -MAJIRA
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)