Text Widget

Recent Posts

Desemba 06, 2013

HII NDIYO KAULI YA MH. ZITTO KUHUSU WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUTANGAZA MSHAHARA WAKE BILA SHURUTI,


                                                           Picha ya zito kabwe
  • WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA.

    WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, amesema mshahara wake kwa mwezi ni sh. milioni sita hivyo watu wanaosema analipwa zaidi ya hizo, wanalengo la kutaka kuharibu jina lake.
     
    Pinda aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo akionesha kushangazwa na watu wanaodai analipwa sh. milioni 30 kwa mwezi. 


    "Hizi ni njama za watu wachache wanaotaka kuharibu jina langu, wanasema najiita Mtoto wa Mkulima wakati nalipwa sh. milioni 30 kwa mwezi si kweli...nalipwa sh. milioni sita tu ambayo ni pamoja na posho," alisema. 



    Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ole, Bw. Rajabu Mbarouk Mohammed (CUF), juu ya mchakato wa vitambulisho vya Taifa kukamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015, Bw. Pinda alisema hadi sasa mchakato huo unaendelea vizuri. 



    "Pamoja na kuchelewa kwake, Serikali imeweza kujitahidi ili kuhakikisha unakwenda vizuri kwa kuwafikia watu wote," alisema. 



    Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, amewataka wabunge kuacha kutanguliza masilahi ya vyama vyao ndani ya Bunge badala yake watangulize masilahi ya Taifa kwa manufaa ya Watanzania wote. 



    Bi. Makinda aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana wakati wa kipindi cha kuchangia Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni Mwaka 2013. 



    "Wabunge mnapaswa kuacha tofauti zenu za kichama ndani ya Bunge ambalo ni chombo muhimu cha kujadili maendeleo ya Taifa na wananchi wake...lipo tatizo la ushabiki wa vyama ndani ya Bunge hasa chama kimoja kinapowasilisha hoja, tunadili kwa pamoja kuijenga nchi yetu," alisema. 



    Akichangia muswada huo, Mbuge wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda (CHADEMA), alisema mchakato wa maandalizi ya kura za maoni si mzuri. 



    "Ni muhimu jamii ipewe elimu ya kutosha...kama muswada huu utapita, tuhakikishe vituo vya upigaji kura za maoni vinakuwepo ndani na nje ya nchi ili kutoa fursa kwa Watanzania waishio nje kupiga kura kama wenzao waliopo nchini," alisema. 



    Naye Mbunge wa Mbozi Magharibi, mkoani Mbeya, Bw. David Silinde (CHADEMA), alisema ni vyema Serikali ianze kuboresha daftari la kudumu kabla ya kuanza mchakato huo kwani kuna Watanzania wengi ambao majina yao hayapo katika daftari. 



    Alisema haziungi mkono Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Bara (NEC) na ile ya Zanzibar ZEC kupewa jukumu la kusimamia mchakato huo badala yake waachiwe wananchi wenye vigezo waombe kusimamia kura za maoni wakiwemo walimu. 



    Muswada huo uliwasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera ,Uratibu na Bunge), Bw. William Lukuvi. --

  • -MAJIRA

0 comments:

Chapisha Maoni