Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwakilalo (25) mkazi wa Block T
alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mbeya
baada ya kupigwa na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria
mkononi kwa tuhuma za kuiba simu.
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa 02:15 usiku huko katika maeneo ya
Block T, jiji na mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa marehemu alikamatwa na
kuanza kupigwa na wananchi hao na badae alipelekwa na kufungiwa katika
ofisi za mtendaji ambapo alitoroka na ndipo wananchi hao walimuona na
kumkimbiza na kuanza kumpiga hali iliyopelekea kumvunja mkono wake wa
kushoto na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Hakuna
mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya. Juhudi za kuwatafuta
waliohusika katika tukio hilo zinaendelea.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed
Z. Msangi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wawafikishe
watuhumiwa wanaowakamata kwa makosa/tuhuma mbalimbali katika mamlaka
husika kwa hatua zaidi za kisheria.
0 comments:
Chapisha Maoni