Text Widget

Recent Posts

Desemba 03, 2013

TAZAMA MUONEKANO MPYA WA MSANII RAY C,BAADA YA KUACHA MADAWA NA KURUDI KWENYE GEMU NI ADIMUUUUUUU!!!!!

 Pichani juu ni mdada Rehema Chalamila ‘Ray C’ na chini ni mashairi ya wimbo mpya anaouandaa mwanadada huyo ambao ameutupia katika ukurasa wake wa Instagram. Mwanadada huyo kwa sasa yupo busy akiandaa nyimbo mpya.
Hivi karibuni wakati akiongea na GPL, Ray C alisema ana singo mpya kama 4 au 5. “Naandaa albamu itayokuwa na ngoma zote kali nilizofanya kwa takriban miaka 10 sasa itaitwa The Best of Ray C. Itakuwa na greatest hits zangu zote nilizofanya kwa kipindi chote hicho. Tumuombe Mungu.

Akinijali na kama mipango itaenda vizuri, Desemba mwaka huu nitarudi rasmi stejini. Nitafanya shoo maalum kwa mashabiki wangu. Nitakuwa na nyimbo mpya kali na zile za zamani. Sipati picha kwa watu watakaohudhuria kwani watapata burudani adimu kutoka kwangu.” Alisema Ray C

0 comments:

Chapisha Maoni