Moja ya kitalu cha kuotesha miche ya miti kilichopo katika kijiji cha Kifanya wilayani Njombe; kitalu hicho ni cha wakulima wanaounda umoja wa wapanda miti Kifanya |
Meneja Mawasiliano wa Mradi, George Matiko akifafanua jambo kwa wanahabari; aliyeketi ni Mkurugenzi wa Programu hiyo, Dk Maria Tham |
Dk Maria Tham katika mahojiano na wanahabari ndani ya ofisi zao zilizopo mjini Njombe |
Mwenyekiti wa kikundi cha wapanda miti wa kijiji cha Kifanya akitoa ufafanuzi wa shughuli zinazofanywa na kikundi chao |
PROGRAMU
ya Panda Miti Kibiashara imeanza kutekelezwa katika wilaya mbalimbali za mikoa
ya Iringa, Njombe na Morogoro.
Wilaya
hizo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Programu hiyo yenye makao yake makuu mjini
Njombe, Dk Maria Tham ni pamoja na Makete, Njombe na Ludewa kwa mkoa wa Njombe.
Wilaya zingine ni Kilolo
na Mufindi kwa mkoa wa Iringa na Kilombero kwa mkoa wa Morogoro.
Dk
Tham alisema lengo kuu la program hiyo iliyoanza Januari mwaka huu ni kuongeza
kipato vijijini kutokana na kupanda miti kitaalamu kwa kutumia mbegu bora na
kuhudumia mashamba ipasavyo kwa kuzingatia mipango ya matumizi endelevu ya
ardhi.
“Uwezo
wa kufikia lengo kuu la program ni mkubwa kwa kuwa katika mikoa ya Nyanda za
Juu Kusini kuna udongo unaofaa kukuza miti, mvua za kutosha, ardhi ya kutosha
na wakazi wake wanapenda kupanda miti,” alisema.
Alisema
kwa kupitia program hiyo mipango ya matumizi endelevu ya ardhi itatengenezwa
huku wananchi wanaopanda miti wakihamasishwa kuunda vikundi vya wakulima wa
miti kwa nia ya kufanikisha shughuli za upandaji miti.
Katika
kipindi cha miaka minne kuanzia sasa wananchi katika wilaya hizo watahamasishwa
kupanda miti katika eneo lenye ukubwa wa hekta 15,000.
“Huku
wakihimizwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato wakati
wakisubiri miti yao ikue na kufikia umri unaofaa kuvunwa,” alisema.
Alisema
biashara ya miti itaongezeka kwa kuzingatia kwamba ifikapo mwaka 2025
inatarajiwa mahitaji ya malighafi viwandani na kuni yataongezeka kutoka mita za
ujazo milioni 1.5 hadi milioni 3.7.
Baadhi ya wakulima wasema wameupokea mradi huo kwa
mikono miwili na wakaahidi kutoa ushirikiano ili malengo yake yafanikiwa kwa
faida yao na Taifa kwa ujumla
0 comments:
Chapisha Maoni