Baada ya kuzunguka kwa muda mrefu raia
huyu wa kigeni ambaye haikufahamika mara moja anatoka nchi gani aliketi
katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kisha akatoa Mkate huku
akiulainisha na Jam na kuanza kula.Alikula Silesi kadhaa lakini alionekana mwingi wa mawazo kila alipotafuna mkate.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Baadae akasukumia mkate na Maji ya Kilimanjaro.Akafunga maji yake akayarudisha ndani ya begi lake.Akaendelea kutafuna Mkate.Akamuuliza mtu aliyekuwa jirani yake vipi unahitaji na wewe nikupatie kidogo na hii ilikuwa ni silesi ya mwisho.
Baada ya kupita muda mgeni huyo aliamua kuondoka eneo alilokuwa ameketi akipata mkate wake wa kila siku.Ghafla nyuma yake akajitokeza askari wa
manispaa ya Moshi (Mwenye t-shirt nyeupe) ambaye ana jukumu la kusimamia
maswala ya mazingira.
Baada ya kufuatilia kwa kina
,ikagundulika kuwa askari huyo alikuwa anamfuatilia mgeni huyo akitaka
kumtia mikononi kwa kosa la kutupa taka ambazo ni vipande vya mikate na
kopo la Jam na kama unavyofahamu sheria za usafi kwa manispaa yetu ya
Moshi.
Globu ya jamii ikabahatika kuona vipande
vya mikate lakini ilipomuuliza askari huyo ni vipi mbona hajamkamata na
kumpeleka kunako husika kama wafanyavyo kwa wabongo wenzao ,askari huyo
ambaye jina lake halikufahamika mara moja alisema anataka kumkamata
lakini hawaelewani lugha huku akidai kuwa yeye kimombo hakipandi
akalazimika kwenda kuomba msaada kwa asakri polisi kata aliyekuwa katika
kituo hicho cha mabasi.
Raia huyo wa kigeni akaondoka zake.Kumbe askari yule wa mazingira aliyeenda
kuomba msaada kwa askari polisi aliyekuwa katika kituo hicho cha mabasi
alikutana na zahama nyingine wakati akiomba msaada kwa asakari huyu
anayeonekana hapa ya kupigwa makofi kwa madai aligoma kwenda kutoa
msaada wa kumkamata yule raia wa kigeni kwa kuwa haujui "Kizungu",na
hapa asakari huyo aliamua kumueleza mwenzake (mwenye t-shirt
nyeupe)aliyetambulika kwa jina la Mkude kuhusu tukio hilo ndipo Mkude
kwa ghadhabu ya hali ya juu akaenda kuwakamata asakari hao wa mazingira.
Wakati asakari hao wa mazingira wakifanya utaratibu wa kumakamata raia huyo wa kigeni ghafla walidakwa na Mkude wote wawili.
Kisha safari ya kwenda Kituoni ikaanza.
Wakati asakari hao wa mazingira wakifanya utaratibu wa kumakamata raia huyo wa kigeni ghafla walidakwa na Mkude wote wawili . |
Kisha safari ya kwenda Kituoni ikaanza. |
Ghafla Mkude baada ya kuona kamera ya globu ya jamii inammulika alimuamuru askari mwenzake kuikamata ,alakini hata hivyo askari yule alifahamu kuwa Globu ya jamii pia iko kazini kama walivyo wao. |
Mzobe mzobe ukaendelea kupita katikati ya kituo kikuu cha mabasi huku mbinje za kutosha toka kwa wakatisha tiketi na wapiga debe zikirindima. |
0 comments:
Chapisha Maoni