Text Widget

Recent Posts

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MSANII. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MSANII. Onyesha machapisho yote

Julai 14, 2014

WEMA AZIDI KUNG'ARISHA NYOTA YA DIAMOND,AZIDI KUTAJWA KWENYE NYIMBO


Mmmh! Hivi Wema alimkosea nini Diamond??? Mbona “kamtaja” tena kwenye wimbo wake mpya???
Leo video ya muziki ya Msanii Diamond platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.

Umri wamponza SHILOLE, akataliwa ukweni



Habari zinadai kwamba baadhi ya ndugu wa msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda ambao ni wakwe wa staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hawamtaki kwa madai kuwa ana umri mkubwa kuliko ndugu yao.

Julai 13, 2014

PICHA ZA DIAMOND PLATNUMZ ALIPOKUWA RED CARPET YA UZINDUZI WA MOVIE YA THINK LIKE A MAN 2



Mtangazaji wa Television kubwa duniani ya E  Terrence J yupo nchini Tanzania ,ambapo pamoja na mambo mengine,alihost uzinduzi wa filamu ya THINK LIKE A MEN TWO,na yeye akiwa mmoja ya nyota walioigiza humo,me na team yangu tulipata mwaliko,na hizi ni baadhi ya picha  tukiingia na  mahojiano ya kwenye red carpet

Julai 12, 2014

KWA WENYE MAHITAJI NA ODA ZA VIDEO SHOOTING,KINKWIN VIDEO PRODUCTION TUNASUPPORT KAZ YAKO

 kinkwi productio ni kampuni inayokuja kwa kasi wapo kimara baruti tembelea kuona kazi zao nzuri walizifafanya wahi mapema kupata hudumu nzuri isiyokuwa na foleni wala usumbufu

Julai 11, 2014

MCHECK KIM NDANI YA KIVAZI CHA BALMAIN 2014


788 67article-2686534-1F87070700000578-212_634x925.jpgyt7utyiuKIM K NDANI YA KIVAZI AMABCHO YEYE HAKUFATA JINSI MAMODO WALIVYOVAA RUN WAY YEYE ALICHUKUA HII LEOPARD SKIRT NA TO KIVYAKE ILA KABAMBA

LYRICS: Izzo Bizness -WALALAHOI

Intro:
Walala hoi…Walala hoi…Walala hoi
Chorus:
Walala hoi sisi ndio Walala hoi (Walala hoi) x 4
moja haikai mbili haikai mbaya wako ni jirani babu (Walala hoi) x 4
Verse 1:
Tunaunga unga maisha yetu ni safari bado tunataabika (Walala hoi) / tunakomaa maisha ni
safari imani ipo bado sisi mbali tutafika (Walala hoi) / tumazaliwa kwenye njaa njaa imetulea
sisi home mali hatujakuta (Walala hoi) / mama Yanga baba Simba upinzani babu ndani yani kila
dakika (Walala hoi) / kupinda ni sheria usishangae huku kwetu mbona imeshazoeleka (Walala
hoi) / hatujasoma dili chafu leta pesa babu hata iwe dili ya kuteka (Walala hoi) / tunaonekana
hatuna maana tunatengwa kona zote twa dharaulika / majina yote sisi Vidampa wapumbavu wezi
majambazi yote wametupachika / Rhumba kali wewe utadata/ soma pata ondoa shaka/ faster
umenipata chafu tatu maisha karata/ maisha bondi kukosa na kupata / jela nyummbani hakuna
kuogopa sheli tunamoka/ sisi machizi kama kaboka/ uchungu wa meno na kucha kamuulize
Ulimboka /
Chorus:Repeat

Juni 22, 2014

HATIMAYE LULU NA JOTI WAFUNGA NDOA KIMYA KIMYA, USIKOSE KUANGALIA NDOA YAO IFIKAPO SAA 4 USIKU ITV.


Hatimaye Msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu afunga Ndoa ya Kimya Kimya na Msanii wa Vichekesho Lucas Mhavile maarufu kama JOTI. Ndoa hiyo ya Kimya imefungwa siku chache zilizopita katika fukwe za Kiota cha Maraha cha Escape 1 Mikocheni
Mchungaji akiwafungisha Ndoa hiyo ambae pia ana kipawa cha Uchekeshaji na MC aitwaye Mc Pilipili.

Juni 10, 2014

umelisikia hili:Baada ya Diamond kurudi mtupu, hivi ndivyo Ali Kiba atakavyo wasahaulisha wabongo, machungu ya Mtv MAMA


DSCN0027
Ali Kiba pamoja na mdogo wake, Abdu Kiba hivi karibuni wanatarajiwa kuwasahaulisha wabongo na story zote za mtv mama, na kuhusu yote yaliyojiri kwa
kuwaletea bonge la show litakalofanyika pale new maisha club jumapili hii.Huu ni ujio mpya wa Alikiba baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuonekana hata kwenye media mbali mbali za hapa bongo,

Juni 09, 2014

Soma hapa:Mchekeshaji Tracy Morgan katika hali mbaya baada ya ajali

tracyMchekeshaji maarufu wa nchini Marekani Tracy Morgan bado yupo katika hali mbaya kiafya kutokana na ajali mbaya ya gari aliyopata mwishoni mwa wiki.
Muigizaji huyo wa vichekesho anakabiliwa na majeraha ya kuvunjika mbavu, pua na mguu baada ya gari aliyokuwa akisafiria kugongwa na gari kubwa na kusababisha ajali mbaya.

Mei 26, 2014

BREAKING NEWZZZZZZZZZZ: MSANII MWINGINE WA BONGO MOVIE TENA AFARIKI DUNIA ASUBUHI HII


Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.
 PICHA: Makatab za GPL

Mei 21, 2014

TAZAMA PICHA YA MASTAA BONGO MUVI WALIOTEMBELEA BBC, UINGEREZA

MASTAA wa filamu za Kibongo, Riyama Ali na Wastara Juma leo wametembelea ofisi za BBC zilizopo nchini Uingereza.
Wasanii hao wapo Uingereza kwa ajili ya kucheza filamu iitwayo 'Ughaibuni'.
Mastaa hao waliondoka nchini wakiambatana na wenzao ambao ni Issa Musa ‘Cloud 112’ na Yvonne Cherryl 'Monalisa'.

KUAMBIANA AZIKWA NA MASWALI MAGUMU 5


Stori: Waandishi Wetu
ADAM Philip Kuambiana amezikwa jana kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku akiacha maswali magumu matano kuhusu maisha, mazingira na hatimaye kifo chake, Risasi Mchanganyiko linakupa moja kwa moja.
Mwili wa marehemu Kuambiana ukiwasili kaburini tayari kwa shughuli za kuusitiri.
Marehemu Kuambiana alifariki dunia Jumamosi iliyopita asubuhi akikimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua tumbo ghafla.

Mei 19, 2014

TAZAMA HABARI KTK GAZETI HILI KUHUSIANA NA SABABU YA KIFO CHA KUAMBIANA SUMU YATAJWA



Stori: OSCAR NDAUKA
KIFO cha ghafla cha mwigizaji na mwongoza filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana  kimeibua mazito ya kutosha, Uwazi limeshika kitu mkononi.
Moja kati ya mazito hayo ni kuwepo kwa madai kwamba marehemu alikula au alilishwa sumu kupitia chakula.

Christian Bella Ft Ommy Dimpozi - Nani Kama Mama.(Official Video)

Christian Bella Obama