|
Msanii
wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku
wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo
Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana
kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali
yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya
na baadae kufariki dunia.
|
Kifo
cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii
mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki
kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na
picha zaidi zitawajia baadae.
PICHA: Makatab za GPL
0 comments:
Chapisha Maoni