Text Widget

Recent Posts

Mei 26, 2014

MBEYA CITY WACHAPWA 2-1 NA FC LEOPARD


Mbeya City Usiku huu imefungwa Bao 2-1 na AFC Leopards ya Kenya katika Mechi yao ya Pili ya KUNDI B la Mashindano ya CECAFA NILE BASIN CUP iliyochezwa huko Khartoum, Sudan.
Hadi Mapumziko, Mbeya City walikuwa nyuma kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Mudde Musa katika Dakika ya 30 na Were Paul, Dakika ya 35.
Bao la Mbeya City lilifungwa na Deus Kaseke katika Dakika za Majeruhi.
Kwenye Mechi ya Kwanza, Mbeya City waliifunga Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 na Mechi yao ya mwisho ya KUNDI B ni hapo Jumatano dhidi ya Enticelles ya Rwanda.

0 comments:

Chapisha Maoni