Text Widget

Recent Posts

Novemba 23, 2013

TAZAMA MSANII WA VICHEKESHO NCHINI ACHEZEA KACHAPO HAPO JANA NI BALAAAA TUPU


MSAII huyu maaruru kwa jina ''Kazi Kijeba'' Leo amechezea kichapo kutoka kwa watu wasiojulikana.

Kutokana na vyanzo vya habari viliieleza Website hii kwamba msanii huyu baada ya kutoka Lokesheni kushut kipindi cha VITUKO SHOW alipitia sehemu kupata mbili tatu kama ilivyo kawaida na desturi kwamba sisi wasanii wa
VITUKO SHOW haturuhusiwi kutumia kilevi muda wa kazi.

Ila msanii huyu alishawahi kuwa na rumasi za hapa na pale kwamba akinywa pombe ni mgomvi na mbishi na hii sio mara ya kwanza kuchezea kichapo mpaka polisi ameshawahi kulala kwa kosa la kutoa matusi hadharani akiwa amelewa..! Hivyo amekuwa akituchafulia jina sana sisi wasanii wa kundi hadi ikafikia hatua tukaitisha kikao kambini na kumuonya suala hili ana akakiri kutorudia tena.

Cha ajabu baada ya siku chache akanywa tena na kutoa matusi hadharani kwa mara nyengine kwa kweli alikoswakoswa kudundwa, Taarifa hizo zilivyotufikia sisi wasanii wenzake tulipanga kumkalisha chini na kuongea naye tena kwa mara nyengine, Tena bila aibu wakati mwingine hututukana hata sisi ila kwakuwa sisi tumemzoea na tunamjua tabia yake humpuuzia.

Leo majira ya saa tisa alasiri alichezea kichapo maeneo ya Usagara Jijini Tanga kwa bahati nzuri alitokea msamaria mwema mwenye pikipiki na kumpa lifti kumtoa eneo la tukio.
Mpaka sasa amesharipoti polisi chumbageni na anaendelea kupata matibabu kambini...


HAPA ni asubuhi akiwa na Msanii wa Bendi maarufu hapa nchini Jahazi Moden Taarab ''Amigo''. Picha hii alipigwa kabla hajachezea kichapo cha mbwa mtoto..


DU! hapa kashikilia R/B ya kuwasaka waliomfunza adabu bila kupenda..! 


Ama kweli dunia hadaa.

source: masai nyotambofu

0 comments:

Chapisha Maoni