JESHI la Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma, jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi ili kumnusuru Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa asifanyiwe fujo. Habari za uhakika kutoka Kasulu zinasema, Dk. Slaa alijikuta katika wakati mgumu baada ya kundi la vijana wanaokadiriwa kuwa kumi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuzua fujo.
Fujo hizo zilitokea kwenye uwanja wa Kiganamo, wakati ambao Dk. Slaa akiwa amebakiza dakika 15 kumaliza kuhutubia mkutano wake.
Baada ya kukatishwa mara kwa mara, Dk. Slaa alishindwa kuendelea na kujikuta kwenye wakati mgumu, huku walinzi wake wakihaha asishambuliwe.
Akizungumza na RAI jana, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema vijana hao walionywa mara kadhaa na polisi kuacha kufanya fujo, lakini walishindwa kutii amri.
“Kwa muda mrefu vijana hao waliagizwa na polisi kuacha kufanya fujo, lakini hawakutii…polisi waliona njia pekee ni kupiga mabomu ya machozi,
“Inasikitisha kwa sababu wale vijana waliondoka eneo la mkutano kama mita 60, wakaanza kurusha mawe hovyo, tunawashukuru polisi kwa hatua walizochukua,” alisema Makene.
Alisema baada ya vurugu hizo, Dk. Slaa alishindwa kuendelea na mkutano wake kabla ya muda kumalizika.
“Ni wazi kama siasa hizi zikiendelea hivi, taifa hili litafika pabaya, wapo wananchi ambao waliamua kufukuza wale vijana…tunajua hivi sasa kuna kundi la watu wanapandikizwa chuki dhidi ya CHADEMA,” alisema Makene.
Alisema Dk. Slaa ameapa kuzunguka nchi nzima kuimarisha chama pamoja na kufungua matawi kama alivyoahidi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Alisema Dk. Slaa na msafara wake, wanaingia katika Jimbo la Buhigwe ambako atafanya mikutano ya hadhara.
“Kesho (leo), tunatarajia kuendelea na mikutano yetu katika jimbo la Buhigwe… taifa hili linaongozwa kwa sheria hatutakubali kuona kikundi kidogo cha watu kinavunja sheria,” alisema Makene.
Alisema kesho, Dk. Slaa ataingia katika Jimbo la Kigoma Kaskazini ambalo linaongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho aliyevuliwa nyadhifa zote, Zitto Kabwe.
“Dk. Slaa amesema haogopi mtu, atakwenda kwenye jimbo la Kigoma Kaskazini bila wasiwasi wowote, licha ya kuwapo na vitisho vingi vya uvunjifu wa amani,” alisema Makene.
Itakumbukwa wiki iliyopita, baadhi ya viongozi wa chama hicho mkoani Kigoma walimshauri Dk. Slaa na msafara wake kuahirisha ziara hiyo kwa sababu za kiusalama.
Source:http://www.udakuspecially.com/2013/12/mabomu-yarindima-mkutano-wa-dr-slaa.html
Desemba 09, 2013
MABOMU YALINDIMA MKUTANO WA DR SLAA KIGOMA,"SOMA HAPA ZAIDI"
Posted on Jumatatu, Desemba 09, 2013 by Unknown
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni