Kama ilivyokuwa imetarajiwa na
wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la
Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu
ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''
Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''
Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''
Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.
Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza.
Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.
0 comments:
Chapisha Maoni