.Baadhi ya warembo wanaoshiriki Shindano la Redd's
Miss Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja
SHINDANO la Redds Miss Kinondoni linatarajia kuwashusha jukwaani warembo 20 watakaowania taji hilo litakalo fanyika Agosti 15, mwaka huu katika Ukumbi wa Escape 1, Mikocheni Dar es Salaam.
SHINDANO la Redds Miss Kinondoni linatarajia kuwashusha jukwaani warembo 20 watakaowania taji hilo litakalo fanyika Agosti 15, mwaka huu katika Ukumbi wa Escape 1, Mikocheni Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi
wa habari jana, Mratibu wa Shindano hilo, Innocent Melleck, alisema warembo hao
tayari wameiva na kinachosubiriwa ni kesho tu kujua mshindi ni nani kati yao.
“Kinachosubiriwa ni siku tu kwani warembo hao
wataondoka na zawadi za kila aina na za kuvutia, pia kuna burudani mbalimbali
ikiwemo Malaika Band wakiongozwa na Christian Bella pamoja na msanii wa kizazi
kipya Young Suma watapagawisha mashabiki” alisema.
Melleck alisema, taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa
sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s
Miss Tanzania, Brigitte Alfred.
Warembo wanaoshiriki shindano hilo wanatoka
vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa
kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti maalumu na watu mia moja
wa kwanza kununua tiketi mlangoni kupata Redd’s Original moja ya bure kabisa.
.Aidha alisema, warembo hao wametunga wimbo
mmoja maalum kwa ajili ya kuhamasisha uzalendo, amani na umoja wa Taifa la
Tanzania, tunawaomba wapenzi wa burudani na tasnia ya urembo nchini kuja kwa
wingi kushuhudia namna warembo wa Kanda ya Kinondoni walivyojiandaa kwa
shindano hili.
Kwa upande wake mkuu wa itifaki wa kamati ya miss
Tanzania Albert Makoye aliwaasa washiriki hao kujiandaa kisaikolojia na kusema
kanda ya Kinondoni kwa mwaka huu inaonyesha kujiandaa vyema zaidi sanjari na
kuwa na warembo ambao ni nadra sana kuwaona popote pale nchini.
Nao warembo wanaoshiriki shindano hilo, walikutana
na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, ambapo kila mmoja alijitamba
ataondoka na taji hilo.
Wadhamini wa shindano hilo ni Redd’s Original, Zanzi, Kitwe General Traders, CXC Africa, Jambo Leo, Clouds FM, Michuzi Media Group, Father Kidevu blog, Gletters Salon, E- FM, Habari Mseto Blog, Picolo Hotel na Uhuru Marathon Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni