Mpiga picha na graphic designer
anayefanya kazi kwenye kampuni ya I-View Studios, ni mwakilishi wa
kwanza kutoka Tanzania aliyetajwa tayari kutuwakilisha mwaka huu kwenye
shindano la Big Brother Africa. Majina bado yanaendelea kutajwa hivyo
tunangoja kufahamu mshiriki wa pili.
Tumepata bahati ya kukutana na Idris.
Ni kijana mwenye vituko sana na ukikaa naye kwa muda mfupi lazima
akuvunje mbavu kwa maneno yake ya papo kwa papo ambayo yatakufanya
ugundue kuwa ucheshi ni kitu alichobarikiwa na mwenyezi Mungu.
Kwa wajihi wake, Idris ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye jumba hilo litakalozinduliwa rasmi Ocotber 5.
0 comments:
Chapisha Maoni