Text Widget

Recent Posts

Septemba 21, 2014

STAMINA:WANAOKOPI WANAJISHUSHA VIWANGO



NA SYLVESTER DAVID
MSANII nyota wa muziki wa Hip Hop nchini,Boniventure Kabogo  maarufu kama ‘Stamina’,amewashauri wasanii chipukizi kuwa na upekee katika kazi zao za muziki nchini.

Akizungumza na TASWIRA HURU BLOG alisema kuwa na upekee kutawasaidia kujitengenezea mazingira na mafanikio makubwa katika muziki,aliyasema hayo kutokana na wimbi la wasanii chipukizi kufanya mziki kama anaoufanya.
\
“Unajua wasanii chipukizi wanatakiwa kujijengea wao utambulisho na upekee wao na siyo kufanya kama msanii Fulani mkubwa,siyo vibaya bali hakutamsaidia yeye kumjenga kimuziki labda mpaka msanii husika afe ndiyo anaweza kuchukua nafasi lakini mbana mimi nampenda Fid Q lakini simkopi au kufanya kama yeye”.alisema.

Stamina ambaye kwa sasa anatamba na wimbo aliomshirikisha msanii Ney Wa Mitego ujulikanao kama ‘Kwenu Vipi’,aliwahi kutamba na nyimbo zikiwemo Kabwela,B52,Pounch after Pounch na Najuta kubalehe.

Pia aliongeza kuwa mashabiki wake watarajie wimbo mpya ambao ni marudio ya wimbo Mpya wa Msanii Fareed Kubanda ‘Fid Q’,ujulikanao kama Bongo Hip Hop,November 14 ambayo itakuwa siku yake ya kuzaliwa.
                        

0 comments:

Chapisha Maoni