Text Widget

Recent Posts

Julai 11, 2014

LYRICS: Izzo Bizness -WALALAHOI

Intro:
Walala hoi…Walala hoi…Walala hoi
Chorus:
Walala hoi sisi ndio Walala hoi (Walala hoi) x 4
moja haikai mbili haikai mbaya wako ni jirani babu (Walala hoi) x 4
Verse 1:
Tunaunga unga maisha yetu ni safari bado tunataabika (Walala hoi) / tunakomaa maisha ni
safari imani ipo bado sisi mbali tutafika (Walala hoi) / tumazaliwa kwenye njaa njaa imetulea
sisi home mali hatujakuta (Walala hoi) / mama Yanga baba Simba upinzani babu ndani yani kila
dakika (Walala hoi) / kupinda ni sheria usishangae huku kwetu mbona imeshazoeleka (Walala
hoi) / hatujasoma dili chafu leta pesa babu hata iwe dili ya kuteka (Walala hoi) / tunaonekana
hatuna maana tunatengwa kona zote twa dharaulika / majina yote sisi Vidampa wapumbavu wezi
majambazi yote wametupachika / Rhumba kali wewe utadata/ soma pata ondoa shaka/ faster
umenipata chafu tatu maisha karata/ maisha bondi kukosa na kupata / jela nyummbani hakuna
kuogopa sheli tunamoka/ sisi machizi kama kaboka/ uchungu wa meno na kucha kamuulize
Ulimboka /
Chorus:Repeat

Verse 2:
Roba za mbao mtaani ni nani kaleta? (Walala hoi) / kulogana logana tu bila sababu mtaani?
(Walala hoi) / majungu fitina unafiki umbea na chuki? (Walala hoi) / kazi ngumu tunapigika
lakini ujira ni mdogo babu (Walala hoi)/ toa kazi tumalize hatulazi kitu hapa sisi mwendo ni wa
CHAP-CHAP/ kwenye Bar hatukai zetu vilabuni yes sisi mwendo ni MATAPU-TAPU / bila
sababu tunakudiss tukijua umetuzidi sisi wala hatukukwepeshi / chuki roho mbaya jadi yetu
Mungu hapendi lakini sisi tumerithi / kila time tupo simple watu wa Mingle mawazo yetu
kwenye Bingo dr.Kingo ngoma zetu ni Segere na Msondo / sisi ndio wachezeshaji tuite Redondo
/ Rest in Peace James mtoto wa Dandu / hii game bado kwako japo upo kando / big brother the
Chase muulize Nando / kama Zay-B vile watu wapo gado /
Chorus:Repeat
Outro: Walala hoi…Walala hoi…Walala hoi…Walala hoi x 3…hoi hoi hoi Walala … hoi hoi
hoi Walala… hoi hoi hoi Walala.

0 comments:

Chapisha Maoni