Ali Kiba pamoja na mdogo wake, Abdu Kiba hivi karibuni wanatarajiwa kuwasahaulisha wabongo na story zote za mtv mama, na kuhusu yote yaliyojiri kwa
kuwaletea bonge la show litakalofanyika pale new maisha club jumapili hii.Huu ni ujio mpya wa Alikiba baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuonekana hata kwenye media mbali mbali za hapa bongo,
jambo lilowafanya baadhi ya fans wa Alikiba na muziki wa bongo fleva kwa ujumla, kujiuliza kama mkali huyu amepotezea muziki au la. Habari zilizo chini ya kapeti zinasema kuwa kiba yuko chimbo sasa hivi akijipanga kwa ujio wake mpya kabisa, na sasa hivi anapasha tu kwa makubwa aliyoandaa kipindi chote alichopotea kwa muda.
0 comments:
Chapisha Maoni