Mchekeshaji
maarufu wa nchini Marekani Tracy Morgan bado yupo katika hali mbaya
kiafya kutokana na ajali mbaya ya gari aliyopata mwishoni mwa wiki.
Muigizaji huyo wa vichekesho anakabiliwa na majeraha ya kuvunjika
mbavu, pua na mguu baada ya gari aliyokuwa akisafiria kugongwa na gari
kubwa na kusababisha ajali mbaya.Baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake, Morgan ameanza kuonyesha matumaini lakini ataendelea kubaki hospitalini kwa wiki kadhaa akipatiwa matibabu, kwa mujibu wa msemaji wake.
Katika ajali hiyo iliyotokea mjini New Jersey muigizaji mwingine wa vichekesho Jimmy Mack, alipoteza maisha.
0 comments:
Chapisha Maoni