Katibu Mkuu Utumishi George Yambesi(kulia) akipewa ushauri nasaha kabla ya kupima VVU kwa hiari wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kuhamasisha Upimaji VVU Mahali pa Kazi uliofanyika mjini Njombe juzi |
Akitoa nasaha zake kwa wawakilishi wa mikoa ya Iringa na Njombe walioshiriki uzinduzi wa kampeni hiyo |
Hilda Kapanda mmoja wa watumishi wa halmashauri ya Njombe anayeishi na VVU akitoa ushuhuda wake |
Huyu Anjela Kayombo ambaye pia ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe anayeishi na VVU tangu mwaka 1999 |
Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wakiwa katika foleni wakisubiri kupima afya zao wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo |
KAMPENI
ya kuhamasisha Upimaji wa Virusi vya Ukimwi mahali pa kazi imezinduliwa kitaifa
mkoani Njombe huku baadhi ya watumishi wenye maambukizi hayo wakilalamika
kutelekezwa.
Kauli
Mbiu ya kampeni hiyo iliyoanza Septemba 23 na itakayofanyika hadi Desemba 1,
mwaka huu inasema “mfanyakazi jitambue, pima mapema, epuka maambukizi mapya,
ubaguzi na unyanyapaa, zuia vifo vitokanavyo na Ukimwi.”
Alipokuwa
akiizindua kampeni hiyo Katibu Mkuu Utumishi, George Yambesi alisema kampeni
hiyo inalenga kutoa msukumo wa utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti Ukimwi
kitaifa na kimataifa ili kufikia azma ya sifuri tatu.
“Sifuri
tatu kwa maana ya maambukizi mapya sifuri, vifo sifuri na unyanyapaa sifuri
ifikapo mwaka 2015,” alisema mbele ya wawakilishi wa mikoa ya Njombe na Iringa
waliohudhuria uzinduzi huo.
Wakati
mkoa wa Njombe unaongoza kitaifa kwa kuwa na asilimia 14.8 ya maambukizi, mkoa
wa Iringa ni wa pili kitaifa kwa kuwa na asilimia 9.1 ya maambukizi.
Alisema
kampeni hiyo inahimiza utekelezaji wa dhati wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia
(MDGs) na maazimio yaliyowekwa kwenye Mkutano Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu
UKIMWI uliofanyika mwaka 2001 Jijini New York, Marekani.
Mbali
na Virusi vya Ukimwi (VVU), Yambesi alisema kwa kupitia kampeni hiyo watumishi
na wananchi wengine watapata fursa ya kupima magonjwa sugu yasio ya kuambuzwa
kama kisukari, shinikizo la damu, moyo, saratani, pumu na kupooza.
Alisema
magonjwa hayo ambayo zamani yalikuwa yakihesabika kama magonjwa yanayowaathiri
zaidi watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi hivisasa yanaoonekana ni ya kawaida kwa
watu wa kawaida.
Yambesi
alisema kutopima afya kuna athari nyingi hasa kupungua kwa nguvu kazi,
kuongezeka kwa gharama za matibabu na kupungua kwa tija inayoathiri ukuaji wa
pato la taifa.
“Ili
kuepuka matatizo hayo kuna kila sababu ya kuhamasiha watumishi wa umma kujali
afya zao na kupima ili wachukue hatua kama wahenga walivyosema kinga ni bora
kuliko tiba,” alisema.
Alisema
katika kutekeleza ya wahenga ni muhimu kupima afya mara kwa mara kunasaidia
kuepuka maambukizi mapya na wale wenye VVU kupunguza athari ya kuambukizi
wengine,” alisema.
Alisema
kwa takwimu za mwaka 2013, Tanzania ina watumishi wa umma zaidi ya
500,000 ambao ni sehemu muhimu ya nguvu kazi ya taifa hivyo wanaohitaji kuwa na
afya bora ili watekeleze wajibu wajibu wao.
“Tumekwisha
weka misingi mizuri ya kulinda afya zetu kwa kuandaa waraka kuhusu Ukimwi na
magonjwa sugu yasio ya kuambukizaa. Ni muhimu kwa taasisi za serikali kutekeleza
maelekezo yote ili watumishi wa umma wawe ni wale wenye afya bora,” alisema.
Alisema
watumishi wanapaswa kuwa wazi baada ya kugundulika na maambukizi ya VVU ili
waweze kupata huduma muhimu ikiwemo ya matumizi ya dawa za kupunguza makali ya
VVU (ARVs).
Watumishi
wawili wa idara ya afya ya halmashauri ya wilaya ya Njombe wenye maambukizi ya
VVU, Anjela Kayombo na Hilda Kapanda walisema pamoja na serikali kusisitiza
mara kwa mara kuwasaidia watu wenye matatizo hayo, ahadi hiyo imeendelea kuwa
hewa.
“Tunajua
serikali inayo sera inayolenga kuwasaidia wenye VVU kwa dawa, lishe na vitu
vingine, lakini sisi hatujawahi pata chochote,” alisema Kayombo.
Kampeni
hiyo inafanywa kwa pamoja na serikali na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambalo
katika uzinduzi huo liliwakilishwa na Getrude Sima ambaye ni Mratibu wa Ukimwi
mahali pa kazi wa shirika hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni