Mmoja kati ya waandaaji wa Serengeti
Fiesta 2014, Musa Hussein akizungumza na na waandishi wa habari kuhusu
Fiesta itakayofanyika Mkoa wa Mbeya uwanja wa Sokoine Jumapili.
LILE bonanza lililokuwa likisubiriwa kwa
hamu na wakazi wa Mbeya, Serengeti Fiesta, sasa linatarajiwa kuanza kutingisha
viunga vya jiji la Mbeya kuanzia tarehe 26 hadi tarehe 28, Septemba mwaka huu.
Akizungumza na vyombo vya habari, mmoja
wa waandaaji wa Serengeti fiesta 2014,Musa Hussein,alisema mwaka huu
wameboresha kwa kuongeza vipengere kadhaa vitakavyofanyika kabla ya siku
yenyewe.
Hussein alisema Septemba 26, siku ya
Ijumaa kuanzia majira ya saa nane mchana kutakuwa na Fiesta Soccer Bonanza
litakalofanyika katika viwanja vya Chuo cha uhasibu(TIA) Mafiati jijini Mbeya.
Alisema katika bonanza hilo
litashirikisha timu nne za mabaa na timu moja ya Chuo cha Uhasibu ambapo
mshindi wa kwanza atajinyakulia Katoni 10 za Bia aina ya Serengeti huku mshindi
wa Pili akiambulia Katoni Tano.
Alizitaja timu hizo kuwa ni Chuo cha
Uhasibu(TIA), Baa ya Kalembo, Baa ya Tugelepo na Mabatini Salalizya baa ambapo
bonanza hilo litaendeshwa kwa mtindo wa mtoano.
Hussein alisema siku itakayofuata
kutakuwa na sherehe kabla ya Fiesta(Pre Party) itakayofanyika katika ukumbi wa
Bab’z Lounge ambapo wasanii wote wakaokuwepo siku ya Serengeti watahudhuria
pamoja na timu nzima ya Clouds media.
Alisema siku hiyo kutakuwa na kiingilio
cha Shilingi 10,000 kwa kila mtu huku watu 50 wa kwanza watapata tiketi bure ya
kuingilia Jumapili kwenye Fiesta yenyewe.
Aliongeza kuwa Usiku wa Jumamosi kuamkia
Jumapili kutakuwa na shindano la kupata waimbaji wa kike(Serengeti super nyota
Diva) ambapo mwenye kipaji anatakiwa kuchukua fomu bure Generation fm.
Alisema mshindi wa kwanza katika
shindano hilo atasafirishwa hadi Dsm kwenye fainali pamoja na washindi wa mikoa
mingine 18 kumpata mshindi mmoja atakayebahatika kuingia THT kupata mafunzo
kutoka kwa Barnaba.
Alisema mshindi huyo pia atapelekwa
Studio kurekodi nyimbo pamoja na kushirikiana kurekodi na Msanii nyota nchini
Diamond.
Aliongeza kuwa Siku ya Jumapili kuanzia
majira ya saa nane mchana kutakuwa na Semina ya kutambua fursa ambapo hakuta
kuwa na kiingilio na mtu yoyote anakaribishwa semina itakayofanyikia katika
ukumbi wa Mkapa.
Alisema kuanzia saa 12 jioni sherehe
nzima zitahamia kwenye viwanja vya Sokoine hadi majogoo kwa kiingilio cha
shilingi 5,000 kwa mtu mmoja.
Akizungumzia kuhusu usalama wa Uwanja
Hussein alisema wamejipanga kuimarisha ulinzi na kuhakikisha sehemu ya kuchezea
mpira(PITCH) haiguswi kwa kuzungushiwa fensi.
Alisema Serengeti Fiesta imeshafanyika
katika viwanja vya Shinyanga naMorogoro sehemu ya kuchezea mpira haijaguswa
kabisa hivyo wanauhakika wa kuulinda uwanja wa Sokoine usiharibiwe.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
0 comments:
Chapisha Maoni