Ugomvi wa kisiasa baina ya jimbo la Iraq la Kurdistan na eneo lilobaki la Iraq, umezidi kuwa mkali.
Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Iraq,
Hoshyar Zebari, mwanasiasa maarufu kabisa wa Kikurd katika serikali ya
Iraq, ameiambia BBC kwamba Waziri Mkuu Nouri Al Maliki lazima aombe
msamaha na abadilishe kauli yake kuhusu Kurdistan.Bwana Maliki hapo awali aliwashutumu wakuu wa Kurdistan kuwa wanawapa hifadhi wale aliowaita magaidi.
Kutokana na hayo, waziri wa mashauri ya nchi za nje pamoja na mawaziri wengine wa Kikurd waliacha kushiriki katika serikali.
Ugomvi hasa ulianza mwezi uliopita pale kiongozi wa Kikurd, Massoud Barzani aliposema kuwa anajitayarisha kwa kura ya maoni kuhusu uhuru wa Kurdistan.
Na Ijumaa ugomvi ulizidi pale Wakurd walipodhibiti visima viwili vya mafuta karibu na mji wa Kirkuk wenye utata.
CHANZO:BBC SWAHILI
0 comments:
Chapisha Maoni