





Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina la
Ally Mwinyi na Kujitambulisha anatokea VIKINDU-Pwani amekamatwa na Jeshi
la polisi kwa Ushirikiano na Madreva wa Wabunge hapa Dodoma kwa tabia
yake Mbaya ya Kutapeli watu.
Kijana huyo amekuwa akijihusisha na
Matukio Mbalimbali ya Utapeli hapa Dodoma kwa nyakati tofauti na kwanji
tofauti na kwa watu tofauti.Utapeli wake amekua akiufanya kwenye Uuzaji
wa Viwanja akijidai yeye ni Dalali wa Viwanja,Pia amekamatwa akiwa na
Fungo "FAKE" za Gari ambazo amekuwa akitumia kutembea nazo na kujidai
yeye ni Dreva wa TASAF amekwama Dodoma hivyo anahitaji Msaada,Kwa
nyakati tofauti Madreva wamekuwa wakikutana naye na kuwaomba masaada na
hatimaye Kupewa fedha za Kumuwezesha Kurudi Dsm alikosema ndio anafanya
kazi ya TASAF.
Lakini hadi jana anakamatwa akiwa kwenye
jaribio la Kumtapeli Dreva wa Mh:Makongoro Mahanga, ameshadanganya
Madreva Wengi na bado amekuwa akionekana Dodoma tofauti na maelezo yake
kuwa anahitaji msaada wa Nauli arejee Dsm tangu Bunge la Katiba
Kuanza,Pia ameshukiwa kutapeli watu wengi fedha likiwamo jaribio la
Kuiba pikipiki eneo la Kituo cha Polisi Dodoma.
Wakati anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Wakati anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Rai,Kama Umetapeliwa hapa Dodoma,tafadhali fika Kituo cha Polisi Dodoma Mjini kwa msaada zaidi.
Na Camera ya Vijimambo blog
0 comments:
Chapisha Maoni