Wananchi wenye hasira, wameteketeza
kwa moto nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Mwika Uuwo, Wilaya ya Moshi
Vijijini mkoani Kilimanjaro, wakimtuhumu kulawiti wanaume wenzake. Hasira
za wananchi hao zilifikia kiwango kisichohimilika baada ya mtuhumiwa
huyo mwenye umri wa miaka 42, kudaiwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye
umri wa miaka 12 kijijini hapo juzi.Wananchi wa kijiji hicho wanamtuhumu
mwanamume huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa kwa sababu za
kitaaluma, kuwa ana tabia ya kuwalawiti vijana kijijini hapo.Habari
kutoka kijijini hapo zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boaz, zilisema kuwa mbali na kuchoma moto nyumba
hiyo, pia walifyeka ekari moja ya shamba la migomba la mtuhumiwa huyo.
Kamanda Boaz alisema jana kuwa tukio la kuchomwa moto kwa nyumba
hiyo lilitokea saa 3:30 usiku na ilipofika saa 6:00 usiku wa kuamkia
jana, nyumba hiyo ilikuwa imeteketea yote.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, wakati wananchi wakiiteketeza nyumba hiyo
na kufyeka shamba lake la migomba, mtuhumiwa huyo anayetafutwa na polisi
hakuwepo ndani ya nyumba hiyo.
“Siyo jambo jema kuchukua sheria mkononi kwa sababu huyu ametenda
kosa halafu mnaokwenda kuchoma nyumba yake, nanyi pia mnatenda kosa la
jinai,”alisema Boaz.
“Kama walijua (wananchi) kuwa huyo mtuhumiwa amerudi na yuko ndani, wangemkamata na kumfikisha polisi siyo kuchoma nyumba. Nchi lazima iendeshwe kwa misingi ya kisheria,”alisisitiza.
Kamanda Boaz alisema kuwa juzi polisi walifika kumtafuta mtuhumiwa huyo
kwa lengo la kumkamata, lakini hawakuweza kumpata na inadaiwa alikuwa
amekimbilia mahali kusikojulikana.
Mwinjilisti mmoja wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
aliyeshuhudia tukio la kuchomwa moto nyumba hiyo, alisema familia ya
mtuhumiwa imehifadhiwa kwa ndugu yake.
“Huyo bwana (mtuhumiwa) ni baba mwenye mke na watoto sita na kabla ya
kuichoma moto nyumba wananchi waliitaka familia yake kuondoka kwenye
nyumba,”alisema Mwinjilisti huyo.
Mwinjilisti huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe kwa kuwa siyo
msemaji, alisema awali saa 1:00 usiku wananchi waliiwasha moto nyumba
hiyo lakini wakatokea wasamaria wema wakauzima
0 comments:
Chapisha Maoni