Wakati
wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis
Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji litaondoka mpaka
kufikia mwishoni mwa wiki hii.Leo hii zimetoka taarifa kwamba kiungo wa
kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji wanaondoka
kwenye klabu hiyo kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili.Shinji
anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund kwa
ada ya uhamisho wa £8m.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani leo hii tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake Dortmund.
Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £12m.
0 comments:
Chapisha Maoni