Spika
wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Dkt. Magret Zziwa (wa
pili kulia) akipewa maelezo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya TICS Paul
Wallace namna kampuni yake inavyofanyakazi ya kupakua na kupakia mizigo
katika bandari ya Dar es salaam wakati wa ziara ya Wabunge wa bunge hilo
walipotembelea ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) jana jijini
Dar es salaam.
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
29/08/2014
Jumuiya
ya Afrika Mashariki iko makini katika kutekeleza majukumu yake na iko
karibu na watu wake kwa kuwahudumia kupitia nchi washirika.
Kauli
hiyo imetolewa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA)
Dkt. Magret Zziwa wakati wa ziara yake alipotembelea ofisi za Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) pamoja na wabunge wa bunge hilo jana jijini Dar
es salaam.
Spika
Dkt. Zziwa alibainisha kuwa lengo la ziara ya wabunge hao ni kujionea
shughuli mbalimbali zinazofanywa na TPA na Bandari ya Dar es salaam kwa
ujumla katika kuhudumia nchi washirka kiuchumi na kujiamii.
“Ni
muhimu kuifanya Jumuiya kuwa imara zaidi kiuchumi na kijamii ili
kuwahudumia watu wetu kwa umahiri na umakini mkubwa katika mahitaji yao”
alisema Spika Dkt. Zziwa.
Wabunge
hao walitembelea maeneo mbalimbali bandarini hapo na kujionea shughuli
zinazofanywa ikiwa ni pamoja na kupakia na kupakua mizigo inapoingia au
kutoka ili kusafirishwa kwenda nchi husika.
Spika
Dkt. Zziwa alisisitiza kuwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
wanahitaji kuona jumuiya yao inavyowajali na kuwahudumia wanapotekeleza
majukumu yao ikizingatiwa kuwa kwa sasa hakutakuwa na urasimu wa
kusafirisha mizigo kutoka nchi moja kenda nyingine kwa kukaguliwa mara
mbili ambapo kwa sasa utaratibu wa Himaya Moja ya Forodha umeanza
kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Akionesha
umuhimu wa uchukuzi na usafirishaji wa mizigo kati ya nchi washirika,
Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki, Dkt. Abdala
Juma Abdulla Saadalla amefananisha bandari, reli na barabara katika nchi
kuwa ni sawa na “moyo na mishipa ya damu” ambapo amebainisha kuwa
Serikali ya Tanzania inaendelea kuboresha reli zilizopo ili ziweze kutoa
huduma kwa wakati.
“Tayari
Serikali kupitia wataalamu wake wa ndani imeboresha vichwa vya treni
nane hadi sasa ambapo vinatarajiwa kuanza kutumika Januari mwakani
pamoja na makasha” alisema Naibu Waziri Saadalla.
Kwa
upange wake Meneja wa Bandari ya Da es salaam Awadh Massawe alipokuwa
akiwaeleza Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki namna TPA inavyofanya
kazi, amesema kuwa kwa mwaka 2013/2014 mizigo inayosafirishwa kutoka
bandarini hapo imeongezeka kutoka tani milioni 4.05 mwaka 2012/13 hadi
tani milioni 4.45 mwaka 2013/2014 ambayo ni sawa na asilimia 9.8.
Massawe
amesema kuwa mizigo hiyo ilisafirishwa kutoka bandari ya Dar es salaam
kwenda nchi za Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Burundi, Rwanda,
Malawi and Uganda kwa kutumia mifumo ya barabara na reli.
Massawe
amesema kuwa bandari ya Dar es salaam imekuwa ni kiunganishi cha
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutumia mitandao iliyopo ya njia ya reli
na barabara.
Kwa
upande wa reli, Massawe amesema kuwa Bandari ya Dar es salaam
inaunganishwa na reli ya kati kwenda Mwanza na Kigoma hali
inayorahisisha nchi za Burundi, Rwanda na Kongo DRC kufikika kirahisi na
TARZARA ambayo inakwenda hadi Zambia.
Kwa
njia ya barabara,Bandari ya Dar es salaam inaunganisha Tanzania na nchi
nyingine kuanzia Dar es salaam kupitia Dodoma/Isaka/Rusumo /Kabanga,
Kigali hadi Bujumbura kwa Rwanda na Burundi, vilevile
Dodoma/Mwanza/Mutukula hadi Kampala Uganda.
Aidha,
Massawe amesema kuwa kwa mwaka 2013/2014 kumekuwa na jumla ya asilimia
30.4 ya mizigo yote ilihudumiwa na bandari ya Dar es salaam.
Massawe
amesema kuwa ongezeko hilo la usafirishaji wa mizigo linatokana na
maboresho yaliyofanywa bandarini hapo kuhusu namna ya usafirishaji wa
mizingo kufuatia mfumo wa Himaya Moja ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki na kuboreshwa kwa taratibu za kibiashara nchini na nchi
inapopelekwa mizigo hiyo.
Naye
Kaimu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lusekelo Mwaseba
alifafanua faida ya mfumo wa Himaya Moja ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuwa unatarajiwa kupunguza gharama za kufanya biashara na
kuondoa urasimu wakati wa usafirishaji mizigo, kupunguza gharama za
kiutawala, kuondoa uwezekano wa rushwa na kuimarisha matumizi ya mifumo
ya mawasiliano (ICT) taktika kubadilishana taarifa miongoni mwa nchi
washirika.
Ziara
hiyo ilijumuisha Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Makamishina kutoka Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, mwenyeji Tanzania
pamoja na Viongozi na watumishi wa TPA.
0 comments:
Chapisha Maoni