Legendary wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ akishow love na Meddy Ahmed ‘Mtoto wa Vitoto’.
Siku chache baada ya ndoa ya Legendary wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mtangazaji mahiri nchini, Gardner Gabriel Habash ‘G Habash’ kudaiwa kuvunjika, gumzo limeibuka kufuatia kunaswa kwa picha za Jide na kijana mmoja (dogodogo) aliyetajwa kwa jina la Meddy Ahmed ‘Mtoto wa Vitoto’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mtoto wa Vitoto huyo amekuwa na urafiki uliotukuka na Jide
kwa muda mrefu kabla na baada ya mtafaruku wa ndoa ya Jide na mumewe
Gardner hivyo kudaiwa kuwa ndiyo faraja ya mawazo ya mwanamuziki huyo
hususan kipindi hiki cha changamoto ya mgogoro wa ndoa yake.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data
kuwa, ukaribu wa Jide na bwa’mdogo huyo ulipitiliza kiasi cha watu wa
karibu na staa huyo kuanza kuhisi huenda wana uhusiano usiofaa.
“Ukaribu wao ulipitiliza hadi kila mtu wa karibu na Jide akautilia shaka, isitoshe kama unavyojua, Jide
si mtu wa kuweka mambo yake hadharani. Mbaya zaidi Jide amekuwa
akimposti dogo huyo kwenye mitandao yake ya kijamii,” kilisema chanzo
hicho.
Meddy Ahmed ‘Mtoto wa Vitoto’ akiwa kwenye ndinga ya 'Jide'.
APEWA NAFASI YA TATU
Wakati paparazi wetu akiendelea kukusanya
data kuhusiana na ishu hiyo, chanzo hicho kilizidi kushibisha maelezo
yake kwa kusema Jide amekuwa akimwandika nambari tatu dogo huyo kwenye
mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu eti wanatafsiri kuwa, maana
yake ni kwanza mumewe (Gardner), ya pili yeye (Jide) na ya tatu ni dogo
huyo.
“Dogo yuko sawa na Jide maana ukitaka kuamini fuatilieni kwa ukaribu mtawaona tu hata katika
mitoko ya Jaydee (Jide). Kuna picha kibao zipo kwenye akaunti yake,
dogo anaonekana akiwa kwenye ndinga (gari) la Jide ingawa dogo yuko
makini kweli na suala hilo, nafikiri wamewekeana mikakati ya kuwa wa
siri,” kilisema chanzo hicho.
Meddy Ahmed ‘Mtoto wa Vitoto’ akipozi nyuma ya ndinga hiyo aina ya Range Rover evoque.
PICHA ZATUA RISASI
Baada ya paparazi wetu kupewa mchongo
huo, alianza kuzisaka picha hizo kupitia vyanzo vyake mbalimbali na
kufanikiwa kuzidaka zikimuonesha bwa’mdogo huyo akijiachia juu ya ndinga
inayodaiwa ni ya Jide katika pozi tofautitofauti.
Kama hiyo haitoshi, kupitia akaunti ya Jide ya Instagram, zilionekana picha
tofauti za dogo huyo, ikiwemo ile ambayo aliiunganisha picha tatu
tofauti, mbili za kwake na moja waliyokuwa ‘klozdi’ na Mtoto wa Vitoto.
JIDE ALIPOTAFUTWA!
Katika kutaka kujua ukweli wa
ukaribu wa wawili hao na kufuatilia mwenendo mzima wa viwanja vyao vya
starehe, paparazi wetu alimvutia waya Jide lakini simu yake
haikupatikana hewani kwa siku tatu mfululizo.
‘Jide’ na mtangazaji mahiri nchini, Gardner Gabriel Habash ‘G Habash’ wakati wakiwa pamoja.
DOGODOGO SASA
Baada ya Jide kutopatikana hewani,
Jumatano iliyopita paparazi wetu alimtwangia simu Mtoto wa Vitoto ili
kumsikia anauzungumziaje ukaribu wake na sista huyo ambapo baada ya
kusomewa mkasa mzima,
dogo alikata simu kwa madai kuwa sehemu aliyokuwa siku hiyo haikuwa
nzuri na kuahidi kumpigia paparazi wetu baadaye lakini hakufanya hivyo
hadi kesho yake (Alhamisi) alipopigiwa tena na gazeti hili na kupokea.
ADAI NI MARAFIKI
Huku akiashiria
sauti ya kutojiamini, dogo huyo alisema yeye na Jide ni marafiki
wakubwa katika mazingira ya kawaida, pia ni shabiki wake kama walivyo
wengine ila ishu ya picha mtu yeyote anaweza kupiga.
Kuhusu kuendesha gari linalodaiwa
ni la Jide, dogo alisema hajawahi ila ameshapiga nalo picha na mtu
yeyote anaweza kufanya hivyo kama ana uhusiano mzuri na mwanamuziki
huyo.
“Jide ni rafiki yangu na mimi ni
shabiki wake wa kawaida. Kwa hiyo hilo siyo tatizo lakini pia kuhusu
gari mimi sijawahi kuendesha gari la Jide lakini nimewahi kupiga nalo
picha kweli kama shabiki mwingine na hakuna shida, ila siyo wapenzi, ni
marafiki tu,” alisema Mtoto wa Vitoto.
ATUMA UJUMBE WA MASIHARA
Baada ya kuzungumza hayo, Mtoto wa
Vitoto alikata simu na baada ya dakika tatu alituma ujumbe mfupi wa
maandishi (SMS) kwenye simu ya paparazi wetu uliosomeka hivi: “Acha
kunizingua mwana.”
Paparazi wetu alipompigia simu kwa
mara nyingine kutaka kujua alikuwa na maana gani, dogo huyo hakupokea
simu na hata alipoandikiwa SMS kwamba atoe ufafanuzi kuhusu ujumbe wake
huo, hakujibu chochote hadi gazeti hili linakwenda mitamboni.
MTOTO WA VITOTO NI NANI?
Mtoto wa Vitoto ni kijana wa mjini tu, si Mbongo Fleva wala si Mbongo Muvi ila inadaiwa
kwa sasa anafanya shughuli zake mkoani Morogoro. Amewahi kuishi
Magomeni, Dar ambapo kwa sasa anadaiwa kuhamia Kinondoni, Dar. Ana asili
ya Zanzibar.
0 comments:
Chapisha Maoni