Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
CHANZO
Usiku wa tukio, Oparesheni Fichua Maovu
‘OFM’ ilikuwa katika harakati za kusaka matukio katika Jiji la Dar,
ndipo ilipokumbana na kelele za watu waliokuwa wakijibizana.
Ilibidi OFM itie timu kwenye nyumba hiyo
na kukutana na chanzo kimoja kilichodai kuwa baba mwenye nyumba hiyo
anadai kumfumania jirani yake na mkewe kitandani.
Mke wa Bw. Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ akiondolewa eneo la tukio.
OFM YATINGA NDANI, YAKUTA MAKUBWA
OFM ilizama ndani ya nyumba hiyo na
kukuta purukushani kali ikiendelea, Yusuf akiwa amepandwa na jazba
ambapo katika kumkurupusha mgoni huyo alijigonga mahali na kuumia usoni.
MWENYE MKE AZUNGUMZA NA OFM
Baada ya mambo kutulia, OFM ilimuuliza Yusuf nini kilitokea mpaka kuwepo kwa tukio hilo, akafunguka:
“Nilikuwa katika harakati za kumchunguza
mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama anachepuka, nikabaini kuna
mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo jirani yangu.
Mgoni akijisafisha uchafu mara baada ya fumanizi .
“Nilipomuuliza mke wangu alikiri,
akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba haiwezekani lakini jamaa
anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane humu ndani.
“Ndipo nilipoamua kumuandaa mke wangu
kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku ya tukio) sitakuwepo na sitarudi
ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi. Baada ya kukamilisha mtego
niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa eneo hilo, Kapteni Makumba na
kumuelezea kinagaubaga.”
...akivaa nguo.
MTEGO WAANDALIWA
“Kapteni Makumba aliwaandaa vijana wake
ambapo kuanzia mishale ya saa mbili usiku walijibanza kwenye kichaka
kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya mawasiliano na mimi.”
JAMAA ATIA TIMU NA KIFURUSHI CHA MACHUNGWA
Yusuf aliendelea kudai kuwa, ilipotimu
saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba Eliza alionekana akikaribia nyumba
ya jirani yake huyo kwa hatua za kunyata na kuangalia kulia na kushoto
kisha akazama ndani huku mkononi akiwa ameshika kifurushi kilichobainika
baadaye kwamba kilikuwa na machungwa kadhaa.
...Mgoni akiomba msamaha.
Alisema muda mfupi baada ya kuingia,
sungusungu mmoja alikwenda kujibanza kwenye dirisha la chumba na kupiga
chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo alimshuhudia Baba Eliza akichojoa
nguo chapchapu tayari kwa mtanange, sungusungu huyo akawatonya wenzake.
SUNGUSUNGU WACHOMOKA KICHAKANI
Yusuf akazidi kusema kwamba wote
walitoka kichakani na kwenda kuvamia chumbani ambapo walimkuta mkewe
aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa sababu alijua majanga yatatokea
muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya hivyo kiaina.
...Timu ya Sungusungu iliyoandaliwa kufichua uovu uliokuwa ukiendelea ikimbana mtuhumiwa kwa maswali.
JAMAA AMPIGIA MAGOTI MWENYE MKE
Baada ya hali kuwa shwari, Kamanda wa
Sungusungu, Kapteni Makumba alianza kumsomea mashitaka jirani huyo
aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na la kusema zaidi ya kuomba radhi
na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye aliyemshawishi na haikuwa amri
yake.
Ilibidi jamaa aniombe radhi, alisema
jirani yangu niko chini ya miguu yako naomba unisamehe sitarudia tena
hiki kitendo kwa kweli siyo amri yangu ni ibilisi tu ndiye aliyeniponza,
nisamehe jirani yako nakupigia magoti unihurumie miye mkosefu,” alisema
Yusuf akimkariri Baba Eliza.
...Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya kitanda iliyochafuliwa na mgoni kwa kinyesi.
APIGWA FAINI
Wakati OFM ikiwepo eneo hilo, sungusungu
walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia Mgosi wa Ndima kwa kitendo cha
kumdhalilishia ndoa yake.
Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio saa
sita na ushee usiku, Baba Eliza alikuwa katika harakati za kumlipa fidia
ya shilingi milioni moja mwenye mke
0 comments:
Chapisha Maoni