Text Widget

Recent Posts

Septemba 24, 2014

AMBWENE MWASONGWAE, MKALI WA NYIMBO ZA DINI AWAPA MAKAVU VIONGOZI WA SIMBA,YANGA NA TFF



SAM_0466


Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Ambwene Mwasongwe Mwamlenga (wa kwanza kutoka kushoto, mstari wa kwanza chini) akiwa na mwandishi wa Mtandao huu Allen Kaijage ( wapili kutoka kushoto katika mstari huo huo) kwenye mechi ya Simba dhidi ya Coastal Union mwishoni mwa wiki
Na Allen Kaijage, Dar es salaam
WAKATI mechi ya Simba na Coastal Union ikiendelea pembeni ya kiti changu alikuwa ameketi muimbaji maarufu wa nyimbo za injili,naye si mwingine ni Ambwene Mwasongwe Mwamlenga.
Ambwene kwasasa anatamba na albamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Misuli ya Imani’ yenye nyimbo kama , Misuli ya imani, Natamani, Ndoa, Upendo, Watoto yatima na nyinginezo.
Wengi wao wanamfahanu Ambwene kama muimbaji ila hawafahamu Maisha yake ya upande mwingine akiwa mshabiki na mkereketwa mkubwa wa mpira wa miguu.
Najua una shahuku ya kujua nini Ambwene Mwasongwe anafahamu kuhusu mpira wa miguu, basi fuatilia mahojiano haya.
SAM_0471 (1)
Mwandishi: Ambwene habari yako?
Ambwene: Safi,  habari yako pia?

Mwandishi: Nimefurahi kukuona hapa leo . Ambwene wewe ni mshabiki wa timu gani?

Ambwene: Kwa Tanzania naipenda sana Simba ila ulaya mimi ni shabiki wa kutupwa wa Chelsea.

Mwandishi: Umeanza kuipenda Simba lini?

Ambwene: Miaka ya 1992

Mwandishi: Wachezaji gani wa Simba wa zamani ambao walikua wanakuvutia?

Ambwene: Dua Said, Abdallah kibadeni na Edward Chumillah

Mwandishi: Wachezaji gani wa simba wa sasa wanakuvutia?

Ambwene: Kiukweli navutiwa sana na Uhuru Seleman, pia Okwi na Kiemba.

Mwandishi: Umeanza kuipenda lini Chelsea?

SAM_0467

Ambwene: Tangu 1997 enzi za kina Gullit, FLO  na Dennis Wise

Mwandishi: Ulishawai kucheza mpira?

Ambwene: Nimecheza sana ila miundombinu ilinikwamisha nisisonge mbele.

Mwandishi: Miundombinu kama ipi?

Ambwene:Viwanja na vifaa vya michezo.

Mwandishi: Una lolote la kuwaambia viongozi wa mpira wa miguu Tanzania?

Ambwene: Ninayo mengi sana ila kikubwa nawaomba viongozi wa simba ,Yanga na TFF waendeshe soka kwa ukweli na uwazi. Unajua viongozi wetu wengi si wakweli, ndio maana timu zetu kongwe hazifanikiwi.

Pia hata Tff kutokuwa wakweli kunafanya timu yetu ya Taifa isisonge mbele .

Mwandishi: Ambwene , ahsante sana

Ambwene: Karibu

0 comments:

Chapisha Maoni