Muungano
wa wasanii wawili wacheshi na wenye vituko kutoka Kigoma, Peter Msechu
na Baba Levo hivi sasa utakuwa ukitambulika kwa jina moja la ‘2mbili Wa
Town’.
Wasanii
hao ambao ukibahatika kukutana nao ni ngumu kuondoka bila kuvunja mbavu
zako, wanatarajia kutambulisha project yao mpya ya pamoja ya ‘2mbili wa
Town’ hivi karibuni.
“Jina
la project linaitwa Tumbili wa town, so kuna vitu vingi ndani ya hiyo
project, sema bado hatujaamua kuielezea project nzima mambo yake ya
ndani na vitu vilivyo kwasababu kuna mshindo mkubwa unakuja wakati wa
kutambulisha hiyo project.” Baba Levo ameiambia Bongo5.
Baba Levo amesema ‘Tumbili Wa Town’ ni kundi la watu wawili yeye na Peter Msechu litakalokuwa likifanya mambo mengi.
“Kwanza kwa kifupi ni kama kundi, ni kundi la watu wawili sema sasa kuna vitu ambavyo tutakuja kuvifanya ambavyo ni vitu vikubwa sana sana kwenye hii industry ya muziki, movie na vitu kama hivyo. So ni kwasababu hatujakuwa rasmi kwaajili ya kuielezea hiyo project ndio maana unaona tunakuwa tunaielezea juu juu , kutokana na watu wanaoisimamia project kusema wanataka wahakikishe vitu vyote vimekaa sawa sawa and then sasa ndio tuitambulishe watu wote wajue ni kitu gani,” alisema Baba Levo.
Ameongeza
kuwa licha ya kuungana na Peter Msechu kwaajili ya project hiyo lakini
kila mmoja bado ataendelea na project zake binafsi za muziki walizokuwa
wakizifanya toka zamani.
“Hii project haiwezi kutufanya tusiendelee na project zetu ambazo
tumekuwa nazo kuanzia mwanzo, bado tutaendelea kuwa na brand zetu zile
zile kama Baba Levo, kama Peter Msechu lakini kwa pamoja tunatengeneza
Tumbili Wa Town”.
Naye Peter Msechu kupitia Instagram aliandika kuhusu project hiyo:
“and our official name is “2MBILI WA TOWN” more project to come ya all
stay tuned…. we on point this year no jokes at all… wengine mnatutukana
ni sawa tunashukuru wengine mnafurahi tunachokifanya pia tunawashukuru..
tunachoamini ni kila mmoja anajua namna anavyo tafuta ugali wake.. hii
ni yetu ili mradi hatuibi wala kukaba mtu basi tunamshukuru Mungu..”
Baba Levo alimaliza kwa kusema kuwa ndani ya wiki mbili au tatu zijazo project ya Tumbili Wa Town itatambulishwa.
0 comments:
Chapisha Maoni