Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani
ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu
hiyo uliofanyika hivi karibuniUongozi
wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo
ndiyo ambao tunautambua, na tutaendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi
mwingine wowote ule.Tunapenda
kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya
TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala
kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji
zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu.
Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake.
Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikiswa katika vyombo husika kwa hatua zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni