Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na mwenzake Gardner Habash (wa pili kulia) wakielekea kizimbani.
Watangazaji hao wakiongozwa na maofisa wa polisi kuelekea mahakamani.
...Wakiingia mahakamani.
MTANGAZAJI
wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM
leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini
Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau amri ya polisi na kutoa
lugha ya matusi.
Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.
Kibonde
na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu
saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa
anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa
kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena.(Picha na Shakoor Jongo / GPL)
0 comments:
Chapisha Maoni