Shindano
la aina yake kwa akina dada wenye makalio makubwa tayari
limewasili nchini ambapo Mpekuzi wetu amekutana na wanaodai
kuwa ni wawakilishi wa shindano lingine ambalo hufanyika kila
mwaka nchini Nigeria ambao wanahangaikia vibali ili lifanyike
baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani kumalizika.....
Shindano
la namna hiyo limefanyika hivi karibuni nchini Nigeria katika
hoteli ya Federal Palace & Casino ambapo mshindi wake
alizawadiwa gari la kisasa....
Mshindi
huyo bi Ijeoma Nnaj alipagawa baada ya kutangazwa kuwa ndiye
mshindi na kusema kuwa japo amejazia vya kutosha lakini
ushindani ulikuwa ni mkubwa kiasi cha kumtia wasiwasi....
Wawakilishi
hao wa kampuni ya Kinigeria iliyoandaa shindano hilo walisema
wanafanya mipango ya kusajili kwa vile lengo lao ni
kulisambaza shindano hilo Afrika nzima....
Mmoja
wa waandaaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Oscar alisema
wanapata vikwazo vingi katika mpango wa kusajili lakini
wanakaribia kurudisha fomu walizochukua kwenye ofisi ya baraza
la sanaa.
0 comments:
Chapisha Maoni