Katika hali isiyo ya kawaida ila imemtokea Rapper anayefanya vizuri katika anga la gospel hip hop huyu si mwengine bali ni Gazuko ambaye sasa hivi anafanya vizuri na video yake ya Acha kulia.
siku kadhaa zilizopita Gazuko alipiga picha akiwa kwenye kifusi cha mchanga na kupost mtandaoni kupitia account yake ya facebook Gazuko Junior nakuandika ujumbe huu
"MPANGO WA LEO MCHANA ULIKUWA HIVI BAADA YA KUAMKA BILA KUWA HATA NA SHILINGI MIA IKANIBIDI NIINGIE MTAANI KUTAFUTA KAZI ILI SIKU IENDE NAMSHUKURU MUNGU NILIPATA KAZI HII NIKAPATA SHILINGI ELFU TATU HII KAZI NILIANZA KUIFANYA SAA NNE ASUBUHI MPAKA SAA KUMI NA MOJA JIONI. "
Ambapo ujumbe huo ulipelekea maon mbali mbali kutoka kwa mashabiki wa Gazuko na wengine kumwambia kuwa jamaa amefulia kwa maana game limemuacha lakin Gazuko amekanusha kwa kusema kuwa hiyo picha aliyoiweka ni kama kiashiria cha wimbo wake mpya utakaofuata baada ya kazi yake ya acha kulia hivyo hiyo style ya kutanguliza hiyo picha ameicopy kutoka kwa Kala Jeremiah.
picha hii ndio aliyoiiga Gazuko na kuamua kupiga yake akiwa anasomba mchanga na kupost mtandaoni na mwisho wa siku ikamletea dharau..hii ni picha ya Kala Jeremiah akiwa na msanii Ney wa mitego ilisambaa kabla ya kuachiwa kwa wimbo wa simu ya mwisho wa Kala.
0 comments:
Chapisha Maoni