ESCO DEE ft RUF B-IFANYE AKILI
CHORUS ifanye akili izungukeee (akili izungukee)
fikiri vikubwa sio vidogoo (cheza na akili, cheza na akili)
Ifanye akiliiiii, hee hee he heeee ifanye akiliiiii, oooh oooooh Oooooh!
VERSE1
fanye akili ya kikwete iwe akili ya Mugabe,
tudharau wazungu nasi tuishi kiubabe,
mana bado wananyonya nchi inaenda kimazabe,
angalau basi kuwasonya mali zetu wasikabe,
ifanye akili ya mafisadi iwe akili ya mapadri,
wasile sana wapunguze midadi nchi tuifaidi,
ili mladi kizazi kijacho nacho kivunie,
kwamba kulikuwa na wazee wenye hekima wasichukie,
ifanye akili ya machangudoa iwe akili ya ma sister,
akili ya teja ibadilike kuwa akili ya ma teacher,
kila siku watoe darasa hathari ya madawa,
ya kulevya vijana kuhasa,
wasije pagawa,
badili akili ya wachawi iwe akili ya rwakatare,
daima wahubiri injiri ili amani itawale,
wachuna ngozi albino geuza wachune waganga wao,
wafanyia upuuzi muungano toa watafte taifa lao!
VERSE 2
ifanye akili ya wabunge iwe akili ya wananchi,
sio kwenye kampeni wavunge, bungeni wahujum nchi,
wasi ishi kwa ajili ya chama wala kimasrahi,
watetee maisha ya vijana, wajawazito wana die,
ifanye akili ya waziri wa afya iwe akili ya madocta,
maana hospital maafa hakuna vifaa wala tiba,
watu wanakufa,
watu wanapukutika,
nani atakae ziba nyufa mda wa uchaguzi ukifika,
ifanye akili ya wasanii iwe akili ya escodee,
waache sifa kujitapa zaidi waongeze bidii,
watafte idea, zipo njia,
sio mapenzi zaidi,
watu wanazidi angamia na ngono ukimwi unazidi,
ifanye akili ya simba yanga iwe akili ya man u,
ili waache kupuyanga kwa maneno ya vidole juu,
watu tunahitaji viwanja zaidi ya ushindi wa ligi kuu,
jenga uwanja, huo ujanja mwisho tutakula mapato tu!
0 comments:
Chapisha Maoni