Pikipiki aina ya Suzuki ikiwa imenasa mbele ya Lori baada ya kugongana uso kwa uso .Ajali
imetokea barabara kuu ya Arusha Moshi ikihusisha Lori aina ya Sacania
lenye namba za Usajili T 137 ATA na pikipiki aina ya Suzuki yenye namba
SU 40262 mali ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini
Moshi(MUWSA).
|
Baada ya ajali hiyo pikipiki ilibaki ikiwa imesimama baada ya kunasa chini ya Lori la mafuta. Mashuhuda
wa ajali hiyo waliuambia mtandao huu kuwa ilitokea majira ya saa 7
katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi na ile itokayo chuo cha
polisi Moshi kuelekea ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya vipimo.Na Dixon Busagaga
|
Katika
ajali hiyo mwndesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la George Lyamuya,
mfanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,
alifariki dunia papo hapo.
0 comments:
Chapisha Maoni