Wizara
ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi
na Vito (TANSORT) inatarajia kufanya semina ya siku mbili ambayo
itahusisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda na Afisa Madini
Wakazi yenye lengo la kujadili utendaji kazi, mafanikio pamoja na
maboresho ya tasnia ya vito na almasi nchini.
Semina
hiyo itakayofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi,
inatarajiwa kuanza Agosti 14, 2014 na kumalizika Agosti 15, 2014.
TANSORT
itaendesha semina hiyo ili kuboresha shughuli za uthamini wa almasi na
madini ya vito kwa lengo la kukokotoa mrabaha, kutayarisha miongozo ya
bei za madini zinazotumika kukokotoa mrabaha, kutoa huduma za
kijemolojia ( Gemological Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati,
kusimamia mauzo ya almasi na madini ya vito ndani na nje ya nchi.
Semina
hiyo itawawezesha washiriki kutoa maoni yatakayowezesha Kitengo hicho
kuboresha huduma za kutoa ushauri wa masoko, ukataji na ukadiriaji
thamani kwa wachimbaji wadogo na wa kati, kufanya utafiti wa masoko na
bei za almasi na madini ya vito, kutunza takwimu za uzalishaji na mauzo
ya almasi na madini ya vito na kusimamia tasnia ya almasi na madini ya
vito nchini.
Kitengo
cha TANSORT kilianzishwa mwaka 1966 malengo yake yakiwa ni pamoja na
kusimamia mrabaha stahiki unaokusanywa na kulipwa serikalini na
kuhakikisha madini ya almasi na vito yanayozalishwa nchini yanapata bei
bora.
Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
12 Agosti, 2014
0 comments:
Chapisha Maoni