Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (wa
pili kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil
Colaso, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya Nishati ya mbadala
kwa wadau wa Mawasiliano ya simu ya GSMA, iliyofanyika jijini Dar es
Salaam jana. Kulia ni Meneja wa Programu wa GSMA Mobile, Ferdous
Mottakin na Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa Towers Services Ltd,
Prakash Ranjalkar.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
(katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil
Colaso, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya matumizi ya Nishati
Mbadala kwa wadau Mawasiliano ya simu kwa kushirikiana na GSMA,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
Airtel Africa Towers Services Ltd, Prakash Ranjalkar.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
(kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel
Tanzania, Beatrice Singano Mallya, baada ya kuzindua warsha ya siku
mbili ya Nishati ya Kijani kwa Mawasiliano ya simu ya GSMA, iliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana
Kampuni
ya mawasiliano ya kimataifa yenye shughuli katika nchi 20 mbalimbali
Asia na Afrika, leo imeshiriki kuandaa semina ya GSMA inayofanyika Dar
es Salaam kwa siku mbili mfululizo tarehe 12 na 13 Agosti 2014 katika
hoteli ya Serena.
Semina
hiyo ya kimataifa ya GSMA inalenga zaidi kutazama maendelea ya sekta ya
Mawasiliano kwa kuangalia Zaidi mipango, mafanikio na fursa ya baadaye
ya mawasiliano ya nishati mbadala rafiki kwa mazingirana yaani –green
telecoms, pia itaendesha majadiliano juu ya mikakati inayowezekana
kuongeza maendeleo katika sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia matumizi
ya nishati rafiki kwa mazingira (green power energy).
Semina
hiyo inahudhuriwa na makampuni kutoka mataifa yapatayo 60 ikiwemo
Tanzania, ambapo wanajadiliana na kubadilishana mawazo katika sekta ya
mawasiano.
Sunil
Colaso, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel alisema, “tunajisikia fahari sana
kushiriki katika mabadiliko ya nishati ya kijani yenye lengo la kutunza
mazingira ambayo yataleta faida kubwa katika jamii yetu. Ushirikiano
wetu na GSMA katika kuandaa tukio hili kutatuwezesha pia kuanzisha na
kuleta technolojia mpya ambapo tutachangia kwa kutoa mawazo yetu katika
mijadala inayohusiana na mawasilano endelevu nchini Tanzania na Afrika
kwa ujumla sehemu yetu ya kwa jamii (CSR)”.
“Mjadala
iliyoandaliwa itajikita zaidi katika mambo yanayohusu teknolojia na
maendeleo yake kama vile ufahamu kwenye teknolojia ya nishati ya jua,
yaani (solar hybrid technologies) au fuel cell technology na nyingine
nyingi. Baadaye, wasemaji mbalimbali wataangazia fursa za uwekezaji na
miundombinu ya biashara ambazo zitaweza kunufaika na uvumbuzi huu wa
matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala–rafiki wa mazingira kutumika
kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania”.aliongeza Colaso
Akiongea
katika ufunguzi rasmi wa shughuli hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa aliwapongeza GSMA na Airtel kwa kazi
yao nzuri katika juhudi za kuleta maendeleo kwa jamii kwa kupitia
teknolojia ya mawasiliano. vile vile alishukuru sana GSMA kuipa nafasi
nchi ya Tanzania kuwa muandaaji wa semina hiyo muhimu kwa mwaka huu. Pia
kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano
hasa kwenye swala la nishati ya kuwezesha minara nchini Tanzania, Prof.
Mbarawa alifurahishwa sana na mtazamo wa fulsa hiyo ya utumiaji wa
teknolojia ya nishati mbadala rafiki wa mazingira.
“kunachangamoto
kubwa katika Kuanzisha na kuendeleza miundombinu kwa kizazi kipya hasa
kwa nchi zetu zinazoendelea. Hivyo, tuna kila sababu ya kukaa na
kushirikiana jinsi ya kutumia teknolojia mbadala ili kwa pamoja
kupunguza changamoto za ukosefu wa nishati, na kuendeleza ufanisi wa
huduma na uhifadhi wa mazingira utakaofaidisha Afrika katika miaka
ijayo” , aliongea Mheshimiwa Mbarawa.
chanzo:full shagwe
0 comments:
Chapisha Maoni