Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kampuni ya Uzalishaji mbegu ya
SEEDCO imezindua mashindano ya mashamba darasa kwa shule za msingi zilizopo
katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo shule itakayolima shamba zuri
itajishindia zawadi ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Frank
Wenga amesema kuwa wameamua kufanya mashindano hayo baada ya
kugundua changamoto kubwa ya elimu katika somo la kilimo ambacho ni uti wa
mgongo wa uchumi wa nchi hii ili kufikia malengo ya kufanya kilimo chenye tija
ni vyema kuwafundisha Watanzania kilimo na wameamua kuanza na wanafunzi
wa shule za msingi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
amesema kuwa shindano hilo ni mahususi kwa shule za msingi zilizopo mikoa ya
kanda ya kaskazini ambayo ni
Kagera,Kigoma,Tabora,Geita,Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Mara.
“Mbali na zawadi kuu ya madawati 100
yenye thamani ya shilingi milioni 15 za kitanzania ,zawadi nyingine zitakuwa ni
sare za michezo,vibao vya kuandikia,madaftari na kalamu na pia mwalimu ambaye
ataifanya shule yake ishinde atazawadiwa simu ya kisasa ya mkononi” Alisema
Meneja huyo
Frank Wenga alisema kuwa fomu za
kujiunga na shindano hilo zitapatikana katika maduka ya mawakala
yaliyothibitishwa kuuza mbegu za Seedco na mwisho wa kujisajili ni August 30
mwaka huu.
“Kampeni hii ya mashindano imelenga
kuwafundisha kilimo kwa njia ya vitendo wanafunzi wa shule za msingi na kutoa
zawadi zitakazowapa motisha ya kupenda kilimo tangu wakiwa shuleni” Alisema
Wenga
Anafafanua kuwa wanafunzi
watajifunza kulima kwa kuzingatia misingi ya kilimo bora cha kisasa ni
pamoja na kutumia mbegu bora,mbolea za kupandia na kukuzia na uhifadhi bora wa
mazao baada ya kuvuna.
0 comments:
Chapisha Maoni