TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga kesho inatarajiwa
kucheza mechi ya kirafiki na Handeni City mchezo unaotazamiwa kuchezwa kwenye
uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa
Ligi kuu Tanzania bara.
Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani hapa,Ofisa habari
wa Coastal Union Oscar Assenga amesema mchezo huo utaanza kesho saa kumi jioni
lengo likiwa ni kujenga undugu baiina ya timu zote mbili.
Assenga amesema katika mchezo huo kikosi kinachotazamiwa kushiriki
ligi kuu msimu ujao kinaonyesha makali yake kwenye mchezo huo.
Aidha mashabikki wa soka mkoani hapa wametakiwa kujitokeza
kwa wingi ili kuweza kushuhudia mchezo huo ambao utakuwa mkali na wa kusisimua.
0 comments:
Chapisha Maoni