Mwanamuziki kwenye muziki wa kizazi kipya Bob Junior hivi karibuni amefunguka na kuweka wazi sababu zilizomfanya aamue kuachana na mke wake.
Katika mahojiano niliyofanya naye kwenye kipindi cha The Takeover, TBC fm, mnamo siku ya Jumanne, Bob Junior alifunguka na kueleza mambo mengi huku akikiri kwamba ni kweli kuwa amemuacha mke wake, "mwanamke anataka kuwa kama mume ndani ya nyumba, amefikia hadi hatua haongei na mama yangu mzazi" alisema Bob Junior.
Nilimuuliza pia juu ya idadi ya taraka alizompa, " mimi nimempa taraka tatu maana nimemaliza kabisa" alisema mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya iitwayo Bashasha aliyomshirikisha Vanessa Mdee.
Novemba 14, 2013
NIMEACHANA NAYE KWA KUMPA TARAKA "3",BOB JUNIOR
Posted on Alhamisi, Novemba 14, 2013 by Unknown
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni