Kikosi
cha timu ya Mtibwa Sugar kilichoanza dhidi ya Yanga SC leo katika
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kushinda mechi ya kwanza Ligi Kuu
Tanzania Bara.Kikosi cha timu ya Yanga SC kilichoanza dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kipa wa Mtibwa Sugar, Saidi Mohames (18) akiokoa moja ya shambulizi la Yanga SC.
YANGA SC imeanza
kwa kipigo cha mabao 2-0 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka
Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro mshambuliaji Genilson Santana
‘Jaja’ akikosa penalti.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa, Dominick Nyamisana wa Dodoma,
aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Milambo Tshikungu wa
Mbeya, hadi mapumziko tayari Mtibwa Sugar walikuwa wanaongoza kwa bao
1-0.
Bao hilo
lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Mussa Hassan Mgosi
dakika ya 16 aliyemalizia pasi ya kichwa ya Ame Ali na kumuwahi kipa Deo
Munishi ‘Dida’ aliyetokea vizuri kutaka kudaka.
Mfungaji wa bao la pili la Mtibwa Sugar ni Ame Ali dakika ya 82 kipindi cha pili.
Yanga SC: Deo
Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan
Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na
Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46.
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL, MOROGORO)
0 comments:
Chapisha Maoni