Wasanii
wa muziki wa Bongofleva Ommy Dimpo na Vanessa Mdee a.k.a Vmoney
wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa mashabiki wa tamasha
la Fiesta 2014 lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora mkoani
Iringa,huku miluzi na shangwe zikisikika kila kona ya uwanja.Tamasha la
Fiesta linatarajiwa kufanyika kesho mjini Morogoro katika uwanja wa
Jamuhuri ambapo wasanii mbalimbali wa bongofleva watatumbuiza.
Baadhi ya Mashabiki wakishangqweka.
Msanii
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva,Selemani Msindi a.k.a
Afande Sele Mfalme wa Rhymes,akiimba kwa hisia kubwa juu ya jukwaa la
tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora
mkoani Iringa.
Msanii wa
muziki wa kizazi kipya Linah Sanga akionesha mumahiri wake kucheza
jukwaani akiwa sambamba na mmoja wa madansa wake mahiri katika tamasha
la burudani la fiesta lililofanyika jana ndani ya uwanja wa samora
mkoani Iringa.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la Fiesta 2014 ndani ya Samora mjini Iringa hapo jana.
Anajiita
Rais wa Manzese,jina lake la kisanii anajiita Madee kutoka kundi la TIP
TOP CONECTIONs,akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Iringa
waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa
Samora hapo jana.Tamasha la Fiesta kesho linatarajiwa kufanyika ndani ya
uwanja wa jamuhuri mkoani Morogoro.
Wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza ndani ya tamasha la Fiesta wakishangweka kwa raha zao.PICHA NA MICHUZI JR-IRINGA.
0 comments:
Chapisha Maoni