Ripota
wa TZA (millardayo.com na AyoTV) Uganda Bill the African ameripoti
kutoka kwenye bunge la nchi hiyo kwamba Wanaume kutoka kaskazini mwa
Uganda wamefikisha maombi kwa Wabunge wao kuhusu ishu ya mipira ya kiume
(Condom)
Hawa Wanaume wanataka Wabunge wao wawaambie wauzaji wa Condoms Uganda
kupeleka saizi kubwa za Condom kutokana na zilizopo sokoni kutowatosha
kwa sababu zina saizi ndogo na ndio maana hawazitumii.
Tom ambae ni Mbunge wa Moyo pamoja na Wabunge wenzake amesema >> ‘Nimeshuhudia
hili kwamba watu wa maeneo hayo wanataka condom kubwa sababu wanauume
mkubwa hivyo condom zilizopo ni ndogo na haziwatoshi kwenye uume….‘ Mbunge mwingine akasema ‘baadhi ya vijana wanalalamika kwamba baadhi ya condom wanazopewa ni fupi na haziwatoshi’
Serikali chini ya mashirika yake itabidi wafanye kazi ya kuongea na
makampuni yenye tenda ya kupeleka condom Uganda ili yalete condom
zinazowaenea Wananchi.
Vilevile mmoja wa Wabunge kwenye bunge hilo la Uganda amewapongeza
Wabunge wenzake kwa sababu condom zinazowekwa kwenye vyoo vya bunge hilo
vinavyotumiwa na Wabunge zimekua zikiisha mapema hivyo kuonyesha kwamba
Wabunge hao ni watumiaji wazuri wa kinga hiyo.
Zaidi unaweza kuplay hapa chini kumsikiliza Bill…
0 comments:
Chapisha Maoni