Rais
wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), Michel Platini amesema Bayern
Munich italazimika kutoa adhabu ya kumsimamisha Franck Ribery kucheza
mechi
tatu iwapo atagoma kuichezea Ufaransa.
Riberry ametangaza kustaafu kuichezea Ufaransa akisisitiza ni wakati wa kuwaachia vijana.Lakini
Platini ambaye ni nyota wa zamani wa Ufaransa amesema mwenye chaguo la
kucheza au la ni kocha, kwamba amtumie yupi lakini mchezaji hawezi
kukataa kuichezea timu ya taifa kama ameitwa.
Kocha wa Les Bleus (Ufaransa), Didier Deschamps amemchagua Ribery kwenye kikosi chake.
'[Kwa Ribery] hana uwezo wa kuamua kujiunga au kutojiunga na timu ya taifa kama kocha wake Didier Deschamps amemuita.
'Hii
iko wazi kwenye kanuni za Fifa, kama akikataa basi Bayern Munich
wanatakiwa kuchukua hatua. Mimi hata simuelewi, Michuano ya Ulaya
itafanyika Ufaransa mwaka 20I6,” alisisitiza Platini.
Kauli
hiyo ya Platini imeonyesha kuwashitua wengi na hasa kuhusiana na suala
la kumlazimisha mchezaji kujiunga na timu ya taifa wakati alijiuzulu kwa
hiari yake.
Ribery
alikosa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil wakati Ufaransa
ilipotolewa kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil
kutokana na kuwa majeruhi.
0 comments:
Chapisha Maoni