WAKATI
suala la Utanganyika na Utanzania liendelea kukuna vichwa vya wanasiasa
na wananchi wa kada mbalimbali Mwanasiasa Mkongwe Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru amewataka watanzania wasahau hilo na kujitambua kuwa wao
ni Watanzania.Kauli
hiyo ya Ngombale Mwiru inakuja ikiwa ni muda mchache baada ya Mjumbe
mwenzake ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Maalumu la Katiba John Cheyo
kusema itakuwa ngumu kwa jamii kuondolewa dhana ya kuwaTanganyika haipo.
Mzee
Ngombale Mwiru alisema ni jambo la kusikitisha kuona watu wanaitaja
Tanganyika wakati wakijua kuwa hiyo ni historia ya aibu kwa Watanzania
ambao walikuwepo katika kipindi hicho cha ukombozi wa Taifa hili.
Ngombale
Mwiru alisema jambo la kushangaza wapo watu ambao hata Tanganyika
hawajaishuhudia lakini wameonekana kuwa na nguvu ya kuhitaji uwepo wake
jambo ambalo linapotosha jamii.
“Kwa
kweli sikuwa na dhamira ya kulizungumzia suala hili ila nimeshawishika
baada ya kuona mzee mwenzangu kuongea na kuonyesha kuhitaji Tanganyika
jambo ambalo mimi nalipinga kwa nguvu zote kwa sababu najua historia
yake haina maana kwa Watanzania wa leo” alisema.
Aidha
Mzee Ngombale Mwiru alitoa wito kwa jamii kusoma historia ya nchi hii
ili kuhakikisha kuwa wanapata takwimu sahihi za nchi yao ili kuacha
tabia ya kufuata mkumbo ambao hauna tija kwa maslahi ya Taifa.
Akichangia
katika Bunge hilo Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo alisema
itakuwa ngumu kuisahau Tanganyika kutokana na ukweli kuwa ndiyo msingi
wa uwepo wa Tanzania.
Cheyo
alisema haiwezekani Zanzibar ikaendelea kuwepo na kutambulika na
Tanganyika ikasahaulika katika mazingira ya kawaida kama baadhi ya
viongozi wengine wanavyotaka.
Mjumbe
huyo wa Bunge la Katiba alisema ni vema jamii ikapatiwa elimu ya
kutosha ili kuhakikisha kuwa ufahamu unakuwepo wa kutosha ili kila
Mtanzania aweze kuwa na uelewa juu ya nchi yao.
Kwa
upande mwingine Cheyo amewataka wabunge kutoka Zanzibar wasije kuzuia
haki za Watanzania Bara wanaozidi milioni 47 wakati wa upigaji kura ili
kuhakikisha kuwa Katiba hiyo inayopendekezwa inapita.
Cheyo
alisema idadi ya wazanzibari ni ndogo ila ina nguvu katika mchakato
mzima wa kupatikana kwa katiba ambayo itaweza kulinda muungano wa nchi
au kuuvunja.
Alisema
lipo suala la aina ya muungano ambalo limeweza kuleta malumbano makubwa
sana katika Bunge hilo hivyo ni vema suala hilo likatafakariwa vizuri
ili kuhakikisha kuwa kila upande unaridhika kwa maslahi ya Taifa.
Cheyo
alisema itakuwa vizuri iwapo fursa itapatikana kwa wahusika kutoa
nafasi kwa wananchi kupiga kura dhidi ya aina gani ya muungano
wanaoutaka ili kuhakikisha kuwa suala hilo limetatuliwa.
Mbunge
huyo wa Bunge la Katiba alitoa rai kwa baadhi ya wanasiasa na
wanaharakati ambao wanaendelea na harakati za kuhamasisha jamii kupinga
Bunge hilo waachane na mpango huo kwani wao wapo kihalali.
Alisema
Kituo Cha Demokrasia (TCD) kipo hivyo wanapaswa kukitumia ili
kuhakikisha kuwa wanafikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na sio
kung’amg’ania maandamano ambayo yanahatarisha maisha ya watanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni