Text Widget

Recent Posts

Agosti 24, 2014

MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO KWA WANAWAKE/WANAUME

LEO tuangalie tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo (Urinary disorders) kwa wanawake na wanaume.
Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa simple cystitis au Bladder infection na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa pylonephritis au kidney infection.

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli. Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.

Lakini watu wengine wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi japokuwa kuna visababishi vingine vichache.Bakteria wa Escherichia coli hawapo peke yao huambatana na waitwao staphylococcus, saprophyti cus, pseudom onas, enterobacter…
LEO tuangalie tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo (Urinary disorders) kwa wanawake na wanaume.

Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa simple cystitis au Bladder infection na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa pylonephritis au kidney infection.


Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli. Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.

Lakini watu wengine wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi japokuwa kuna visababishi vingine vichache.Bakteria wa Escherichia coli hawapo peke yao huambatana na waitwao staphylococcus, saprophyti cus, pseudom onas, enterobacter n.k.

Maambukizi katika njia ya mkojo  lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo  na si pengine popote. Wapo wanawake wamekuwa wakiniuliza kuhusu tatizo la kutokwa na uchafu ukeni na kudhani ni ugonjwa huu, huo ni ugonjwa tofauti kabisa na huu tunaouchambua leo.

Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo, tuna maana ni kutoka eneo la nje la utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalamu huitwa Lower Urinary Tract Infect na ikihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.

Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake hutokea wakati wa kujisafisha, kutonawa vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani chafu. Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bakteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi.

Upungufu wa homoni ya kike iitwayo Oestrogen husababisha bakteria wasababishao maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi.Matatizo haya ya maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake, huwakumba pia watoto wadogo kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi, njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani.

Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao hupata maambukizi rahisi kutokana na viungo vyao vya uzazi kuwa vifupi na wanaponawa maji yasiyo salama kwa watoto wa kiume huwa rahisi bakteria kubaki katika ngozi inayoning’inia (govi), hivyo kusababisha tatizo hili.
Lakini pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambuzi kutokana na sababu ambazo tumezitaja hapo juu ambapo pia ni rahisi kwao kuambukizwa Ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana tunasisitiza tohara kwa wanaume.

Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo zaidi ni bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kusafiri kwa bahati mbaya  na kujikita katika mfumo wa mkojo. Bakteria wengine waambukizao njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia na trimonas na fangasi wanapojamiiana bila kutumia kinga.

Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo, mara kwa mara, ni vema kutumia kinga yaani kondomu na kwa mwanamke kila anapomaliza kufanya ngono akojoe ili kuondoa bakteria walioingia au waliokaa katika tundu ya mkojo wakisubiri kuingia.Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu, unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha huchangia tatizo hili.

Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo hata ndani ya kibofu pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.
Dalili
Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa, mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali japokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo au wengine huita UTI yaani urinary tract infection wana ugonjwa huu.

Dalili nyingine za maambukizi ni maumivu,  kutokwa na usaha au majimaji wakati wa kukojoa kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi moto wakati wa kukojoa mkojo.

Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.

Wengine wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo, au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.Mgonjwa anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu, kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili kuonesha kushoka.

Wagonjwa wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu  ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi.Matatizo haya ya mfumo wa mkojo kama tulivyoona huko juu huwapata watu wote wanawake na wanaume. 
Watu wenye  matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI. Kwa wanaume huhisi hata nguvu za kiume kupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo la ndoa.
WAJAWAZITO
Kwa wajawazito ugonjwa unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni. Bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhara mengine kama vile  shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo.

TIBA
Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin, Fosfomycin, Monurol, Furadantin, Sulfam ethoxazole, co-trimax, ampicillin, gentamicin na kadhalika lakini usitumie dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.

Ushauri
Tunashauri kwa mwanamke kwamba epuka kujisafisha sehemu za siri na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.

Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo.
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi.

Kwa mwanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kujipenyeza hadi katika korodani na huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kukufanya uwe mgumba.
Maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume (prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi. Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.


0 comments:

Chapisha Maoni