MCHEZAJI
kutoka Cameroon amekufa baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki
waliokereka waliporusha mawe mwisho wa mechi ya Ligi ya Algeria.
Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyefunga mabao mengi katika Ligi ya Algeria msimu uliopita.
Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kuwa timu yake, JS Kabylie, iliposhindwa kwa mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou.
Marehemu ndiye aliyefunga bao hilo pekee kwa timu yake.
Wizara ya mambo ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe kuhusiana na kifo hicho.

0 comments:
Chapisha Maoni