Text Widget

Recent Posts

Agosti 09, 2014

KOCHA WA YANGA AWAZUNGUMZIA WACHEZAJI WAKE WABRAZIL


Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonaldo Leiva amesema ushirikiano na juhudi ndiyo utaisaidia Yanga kufanya vizuri na si kuamini baadhi tu wanaweza kuwa msaada kwa kikosi chao.
Leiva raia wa Brazil amesema iwapo kila upande utafanya kazi yake kwa asilimia mia, Yanga itafanikiwa lakini si kuamini kundi fulani ndilo lenye msaada.
“Ukisema Wabrazil wamekuja basi Yanga itafanya vizuri, tutafeli. Lazima tufanye kazi kwa juhudi kubwa kipindi hiki cha maandalizi na itakapoanza ligi.
“Pili ni ushirikiano, lazima uwe ni wa juu sana na kila mmoja ampende mwenzake kama familia,” alisema.
Yanga imeajiri Wabrazil wanne na kuweka rekodi mpya ya Wabrazil wanne kufanya kazi timu moja kwa wakati mmoja.
Wabrazil hao ni Kocha Mkuu Marcio Maximo, Leiva na wachezaji Coutinho na Jaja.

0 comments:

Chapisha Maoni