Text Widget

Recent Posts

Novemba 23, 2013

TAZAMA AHADI YA BASATA KWA WASANII

Msanii wa muziki wa kizazi kipya  na mwenye tuzo kibao za kimataifa Ambwene Yesaya AY.
Wajumbe wapya wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), wametaka kupewa miezi sita, wasanii waanze kufaidi matunda yao.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzake wa  bodi hiyo iliyozinduliwa juzi, Alex Msama alisema Basata kuna changamoto nyingi ikiwemo kukosa vyanzo vya kutosha vya mapato hivyo changamoto kubwa iliyopo mbele yao ni kuhakikisha Basata inajiendesha yenyewe.
“Tutaboresha kazi za wasanii kwa kuziinua na kuzilinda kwa nguvu zote, tutasimamia studio zitoe kazi bora za wasanii sio bora kazi, tunataka ifike mwisho wasanii kwenda kurekodi Afrika Kusini, China na kwingineko na kazi zetu zivuke mipaka.
“Ndani ya miezi sita, matunda yetu yataanza kuonekana, kikubwa tunaomba ushirikiano kwa wasanii na wadau wote wa Sanaa.”alisema Msama.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Basata, Profesa Penina Mlama alisema anasikitishwa na vitendo vya mmomonyoko wa maadili unaofanywa na wasanii ambao ni kioo cha jamii na badala yake wamekuwa ni wachafunzi wa maadili.
“Kuna umuhimu wa kuendesha kampeni ya kitaifa nchi nzima  kupinga ubomoaji wa maadili na kuelimisha wasanii pamoja na hadhira yao na watanzania kwa ujumla kuhusu umuhimu wa sanaa katika kujenga maadili ya taifa.
Mwananchi

0 comments:

Chapisha Maoni