Owino ni beki tegemeo katika safu ya ulinzi ya Simba sc
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
NAHODHA wa Simba, Mganda, Joseph Owino amesema wachezaji wa klabu
hiyo hawajakata tamaa kwa matokeo waliyopata katika mechi mbili za ligi
kuu soka Tanzania bara.
Simba ilitoka sare ya 1-1 na Polisi Morogoro katika mechi ya raundi
ya pili ya ligi kuu iliyopigwa jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Katika dakika 50 Danny David Mrwanda alifunga goli la kusawazisha
baada ya mabeki wawili wa Simba, Masoud Nassor ‘Cholo’ na nahodha Joseph
Owino kugongana na kumuacha nyota huyo wa zamani wa Simba akifunga.
Kabla ya mechi hiyo, Septemba 20 mwaka huu, Mnyama aliambulia sare ya
2-2 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu uwanja
huo huo wa Taifa.
Kipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio
mpira ulipigwa na Okwi na hatimaye Simba kuandika bao la kuongoza
Baada ya matokeo hayo, Owino alisema: “Tumeanguka kwa mara ya pili,
lakini nadhani bado hatujakata tamaa. Tutaendelea kujituma zaidi mpaka
tupate ushindi”.
“Hakuna makosa, sababu ni kwamba ligi ndio inaanza, timu zinashindana kupata pointi, lakini tunajipanga kufanya vizuri’.
Simba walianza mechi kwa kutawala safu ya kiungo ambapo Jonas Mkude
alionesha kiwango kizuri. Alitawala dimba la kati, alikuwa na jeuri,
alipiga pasi sahihi na kuipandisha timu juu, lakini mambo yalibadilika
kipindi cha pili.
Mkude alionekana kuchoka, wakati huo huo Piere Kwizera, Shaaban
Kisiga, Emmanuel Okwi waliokuwa mbele yake walishindwa kurudi nyuma
ipasavyo na kuisaidia timu.
Kuhusu safu ya kiungo, Owino amekiri kwamba haifanyi vizuri, lakini anaamini kocha Patrick Phiri atafanya kazi.
Owino alisema: “Safu ya kiungo haichezi vizuri sana, lakini mwalimu atafanyia marekebisha na tutacheza vizuri zaidi”.
Wekundu wa Msimbazi watacheza mechi ya raundi ya tatu Oktoba 4 mwaka huu uwanja wa Taifa dhidi ya Stand United.
0 comments:
Chapisha Maoni